Msanduku

(Elekezwa kutoka Tetraclinis)
Msanduku
Msanduku wa Afrika Mashariki (Cupressus lusitanica)
Msanduku wa Afrika Mashariki (Cupressus lusitanica)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Gymnospermae (Mimea isiyotoa maua)
Divisheni: Pinophyta (Miti iliyo na matunda kwa umbo wa koni)
Ngeli: Pinopsida (Miti kama msonobari)
Oda: Pinales (Miti kama msonobari)
Familia: Cupressaceae (Miti iliyo na mnasaba na msanduku)
S.F. Gray
Ngazi za chini

Nusufamilia 7, jenasi 29:

Misanduku ni miti ya familia Cupressaceae katika oda Pinales (mikoni). Spishi fulani huitwa mreteni (Juniperus), msekwoya (Sequoioideae) au msuja (Thuja na Tetraclinis).

Maelezo

hariri

Miti hii inaweza kuwa mifupi na kama vichaka (urefu wa mita kadhaa), mirefu sana na kufikia hadi m 116 au urefu wowote katikati. Hubeba maua ya kiume na ya kike kwenye mti mmoja au kwenye miti tofauti. Gome la miti iliyokomaa kwa kawaida lina rangi ya kahawiamachungwa hadi kahawianyekundu na umbile lake ni la nyuzinyuzi. Mara nyingi linatoa mabamba au linabanduka kwa papi za wima. Katika spishi fulani gome ni laini, lina magamba au ni gumu lenye mipasuko ya umbo la mraba.

Majani yamepangwa ama kwa mazongomo au kwa jozi zinazoelekeana na kila jozi kwa 90° hadi jozi iliyopita au kwa mizingo ya matatu au manne kulingana na jenasi. Kwenye miti midogo majani ni kama sindano na kuwa madogo na kama magamba kwenye miti iliyokomaa ya jenasi nyingi. Jenasi na spishi kadhaa huhifadhi majani kama sindano kupitia maisha yao yote. Majani chakavu hayamwagwi moja kwa moja kwa kawaida lakini katika rasharasha za majani (cladoptosis), isipokuwa majani kwenye machipukizi ambayo yatakuwa matawi. Majani haya huanguka hatimaye kila mmoja wakati gome linapoanza kutoa mabamba. Mingi sana ya miti hiyo ni kijani mwaka mzima na ina majani yanayoendelea miaka 2 hadi 10, lakini jenasi tatu (Glyptostrobus, Metasequoia na Taxodium) huangusha majani kila mwaka au zina spishi zinazoangusha majani.

Koni za mbegu ni kama mbao, kama ngozi au (katika Juniperus) kama beri zenye nyama, na zina chembekike moja au kadhaa kwenye kila gamba. Gamba la kilindaua na gamba la chembekike yameungana isipokuwa kwenye ncha, ambapo gamba la kilindaua huonekana mara nyingi kama mwiba mfupi juu ya gamba la chembekike. Kama ilivyo majani, magamba ya koni hupangwa kwa mazongomo, kwa jozi zinazoelekeana au kwa mizingo kulingana na jenasi. Mbegu ni ndogo na bapa kwa kawaida na yana mabawa mawili membamba, moja chini kila upande wa mbegu. Mara chache tu (k.m. Actinostrobus) kato la mbegu ni pembetatu na kuna mabawa matatu. Katika jenasi fulani (k.m. Glyptostrobus na Libocedrus) bawa moja ni kubwa sana kuliko ingine, na katika nyingine kadhaa (k.m. Juniperus, Microbiota, Platycladus na Taxodium) mbegu ni kubwa na hazina mabawa. Kwa kawaida miche huwa na kotiledoni mbili lakini hadi sita katika spishi nyingine. Koni za mbelewele zinafanana zaidi katika muundo kupitia familia hii. Zina urefu wa mm 1-20 na zina magamba yaliyopangwa kwa njia sawa na katika koni za mbegu. Zinaweza kubebwa peke yao kwenye ncha ya chipukizi (takriban jenasi zote), kwenye makwapajani (Cryptomeria), kwa mafundo mazito (Cunninghamia na Juniperus drupacea) au kwenye chipukizi zinazoning'inia na kufanana na panikali (Metasequoia na Taxodium).

Msambao

hariri

Cupressaceae ni familia ya mikoni inayosambazwa kwa upana yenye msambao wa takriban duniani kote katika mabara yote isipokuwa Antaktiki, unaoenda kutoka 71° N katika Norwei ya Aktiki (Juniperus communis) kuelekea kusini hadi 55° S katika kusini kwa Chili (Pilgerodendron uviferum). Juniperus indica unafika mwinuko wa m 5200 huko Tibet na ndio mwinuko wa juu kabisa umeripotiwa kwa mmea wowote wa mbao. Makazi mengi sana kwenye nchi kavu yamechukuliwa, isipokuwa tundra mbele ya mizingo wa Aktiki na Antaktiki na misitu ya mvua katika tambarare za tropiki. Hata hivyo spishi kadhaa ni sehemu muhimu za misitu ya mvua wastani na za misitu ya mawingu ya nyanda za kitropiki. Miti hiyo pia ni nadra katika majangwa, kwa sababu spishi chache tu zinaweza kuvumilia ukame mkali, hasa Cupressus dupreziana]] wa Sahara ya kati. Licha ya msambao mpana wa ujumla, jenasi na spishi nyingi zinaonyesha misambazo iliyofinyika sana, ambayo mara nyingi inabaki tangu zamani, na nyingi ni spishi zilizo hatarini mwa kutoweka.

Katika Afrika spishi 14 za asilia zinapatikana huko kaskazini hasa. Lakini spishi nyingine kutoka mabara mengine zilipandwa Afrika ili kuvuna ubao wao au kurembesha bustani.

Spishi za kienyeji za Kiafrika

hariri

Spishi zilizopandwa katika Afrika

hariri
  NODES
Idea 8
idea 8