Watitani (kutoka Kigiriki: Τiτᾶνες , titânes - "wanaojikazia") walikuwa nasaba ya pili ya miungu katika mitholojia ya Kigiriki. Jina hilo linataja idadi ya miungu 12 ambao, katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale, walikuwa watoto wa Gaia na Uranos.

Kichwa cha mmoja wa Watitani, Jumba la kumbukumbu la Akiolojia, Athini, Ugiriki

Katika imani ya Wagiriki wa Kale walitawala ulimwengu kabla ya nasaba ya miungu wa Olimpos, ambao walipigania udhibiti wa ulimwengu katika mfululizo wa vita kadhaa unaojulikana kama vita ya Watitani (titanomachy). Waolimpo walishinda na Waitani wengi walifukuzwa mbinguni na kufungwa katika vilindi vya Tartaro.

Watoto wa Uranos

hariri

Kizazi cha kwanza cha Watitani walikuwa wana wa Gaia na Uranos wanaoitwa pia Watitani wazee; walikuwa kumi na wawili kwa jumla.

  1. Hyperion – mungu wa nuru na jua, aliyemzaa mungu wa jua Helios, mungu wa kike wa mwezi Selene na mungu wa kike wa mapambazuko Eos
  2. Iapetosmume wa Klymene (binti wa Okeanos), aliyefukuzwa baadaye mbinguni
  3. Koios, aliyefukuzwa baadaye mbinguni
  4. Kreios – mume wa Eurybia
  5. Kronos – mkuu wa Watitani, baba wa Zeus, mume wa Rhea; alipinduliwa na Zeus akafukuzwa mbinguni akitawala kisiwa cha heri
  6. Mnemosyne – mama wa Muzi tisa
  7. Okeanos – mkuu wa bahari na himaya ya maji, baba wa miungu yote ya mito na pepo wa bahari na visima
  8. Phoibe – mke wa Koios, mungu wa mwezi
  9. Rheamama wa Hestia, Demeter, Hera, Hades, Poseidon na Zeus; alimfuata mumewe Kronos alipoondoka mbinguni
  10. Themis – mungu wa kike wa haki na mke wa pili wa Zeus; anajua wakati ujao
  11. Tethys – mke wa Okeanos
  12. Theia – mke wa Hyperion

Kizazi cha pili

hariri

Kizazi cha pili cha Watitani walikuwa watoto wa wale kumi na wawili wa asili. Hao ni pamoja na watoto wa Okeanos na Tethys: potamoi waliotazamwa kama miungu ya mito, na Okeanidi, ambao walikuwa pepo wa bahari elfu tatu kwa idadi, na vilevile Nephelai, waliokuwa mapepo ya mawingu.

Basi kulikuwa na uzao wa Koios na Phoebe: dada Asteria na Leto .

Baadaye walikuja watoto ambao Hyperion alizaa na Theia : Helios (Jua), Selene (Mwezi), Eos (Alfajiri).

Baadaye wakaja wana wa Iapetos na Okeanidi Asia / Klymene:Atlas (mkubwa), Prometheus na Epimetheus (ambao walikuwa mapacha), na Menoitios .

Mwishowe watoto wa Krios na Eurybia (binti wa Gaia na Pontu ) walikuwa wa mwisho: Pallas, Astraeus, na Perses. Perses angeendelea kumwoa Asteria akizaa naye Hekate, mungu wa uchawi.

  NODES