Vincent wa Lerins

Mtakatifu na mwanatheolojia

Vincent wa Lerins (kwa Kilatini, Vincentius; alifariki 445 hivi) alikuwa mmonaki padri nchini Galia (leo Ufaransa), maarufu kwa maandishi yake ya teolojia na kwa juhudi zake za kufanya imani ya Wakristo istawi ndani mwao[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 24 Mei[2].

Maisha

hariri

Vincent alizaliwa Toulouse. Baada ya kujitafutia maendeleo katika jamii, labda kama askari, aliamua kuingia monasteri ya Lérins kwenye kisiwa Saint-Honorat.

Akitumia jina bandia la Peregrinus aliandika huko Commonitorium (mwaka 434 hivi, yaani miaka 3 baada ya Mtaguso wa Efeso). Sawa na mtaguso mkuu huo, Vincent alitetea matumizi ya jina Mama wa Mungu kwa Bikira Maria, akipinga hoja za Nestori wa Konstantinopoli.

Eukeri wa Lyon alimsifu kama mtakatifu mwenye elimu na ufasaha mkubwa.

Gennadius wa Massilia aliandika Vincent alifariki chini ya makaisari Theodosius II na Valentinian III, kwa hiyo si baada ya mwaka 450. Masalia yake yanatunzwa huko Lérins.[3]

Commonitorium

hariri

Lengo la Vincent katika kuandika Commonitorium[4] lilikuwa kubainisha vigezo vya kutofautisha ukweli wa imani Katoliki na uzushi, ili aweze kujikumbusha (ndiyo maana ya kichwa jicho).

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/54550
  2. Martyrologium Romanum
  3. "Butler, Alban. The Lives or the Fathers, Martyrs and Other Principal Saints, Vol.V, by the Rev. Alban Butler, D. & J. Sadlier, & Company, (1864)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-28. Iliwekwa mnamo 2014-09-28.
  4. Available at http://www.ccel.org/ccel/schaff/npnf211.iii.html

Marejeo

hariri
  • Thomas G. Guarino, Vincent of Lerins and the Devolopment of Doctrine. Grand Rapids: Baker Academic, 2013.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES