Kivinjari

(Elekezwa kutoka Vivinjari)

Kivinjari (kwa Kiingereza: browser) ni programu ya kompyuta inayowezesha kupata habari kupitia intaneti. Kila ukurasa wa intaneti, picha na video, uliounganishwa na wavuti huwa na anwani inayoitwa Kioneshi Sanifu Rasilimali KISARA (Uniform Resource Locator; kifupi: URL). KISARA/URL huwezesha vivinjari kutafuta na kupata maudhui haya kutoka kwa seva ya wavuti na kuyaonyesha kwenye kompyuta ya mtumiaji.

Kivinjari cha wavuti si sawa na injini ya utafutaji, ingawa hizo mbili mara nyingi huchanganywa. Kwa mtumiaji, injini ya utafutaji ni wavuti tu, kama vile google.com, ambayo huhifadhi data inayotafutwa kuhusu wavuti nyingine. Lakini ili kuunganishwa na seva ya wavuti na kuonyesha kurasa zake za wavuti, mtumiaji lazima awe na kivinjari cha wavuti kilichosanikishwa kwenye kifaa chake.

Kufikia Machi 2019, zaidi ya watu bilioni 4.3 hutumia kivinjari, ambacho ni karibu 55% ya idadi ya watu ulimwenguni.

Vivinjari maarufu zaidi ni Chrome, Firefox, Safari, Internet Explorer, na Edge.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Intern 1
mac 1
os 4