Wafiadini wa Vietnam

Wafiadini wa Vietnam ni kundi la Wakristo 117 waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Kati yao kuna maaskofu 8, mapadri 50 na walei 59.

Upande wa asili, 96 ni wenyeji wa Vietnam, 11 ni Wadominiko kutoka Hispania, na 10 wamisionari kutoka Ufaransa.

Kuhusu namna ya kuuawa, 75 walikatwa kichwa, wengine walinyongwa au kuchomwa moto hadi kufa, wengine walikatwa vipandevipande na wengine walikufa baada ya kuteswa vikali.

Katika liturujia wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba.

Wanawakilisha pia wafiadini wenzao wasiojulikana, ambao wanahistoria wa Kanisa Katoliki wamekadiria kuwa kati ya 130,000 na 300,000.

Majina ya wanaojulikana

hariri

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri


Marejeo

hariri
  • Les Missions Etrangères. Trois siecles et demi d'histoire et d'aventure en Asie Editions Perrin, 2008, ISBN 978-2-262-02571-7
  • "St. Andrew Dung-Lac & Martyrs", by Father Robert F. McNamara, Saints Alive and All God's Children Copyright 1980-2010 Rev. Robert F. McNamara and St. Thomas the Apostle Church.
  • "Vietnamese Martyr Teaches Quiet Lessons", By Judy Ball, An AmericanCatholic.org Web Site from the Franciscans and St. Anthony Messenger Press.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES