Where We Are ni albamu ya kundi la Westlife iliyotolewa tarehe 27 Novemba 2009, nchini Eire na tarehe 30 Novemba 2009 nchini Uingereza kupitia studio za Syco Music.

Where We Are
Where We Are Cover
Studio album ya Westlife
Imetolewa 27 Novemba 2009
(See Release History)
Imerekodiwa Julai - Oktoba 2009
Aina Pop, ballad, Pop rock
Urefu 52:05
Lebo Syco Music, Sony Music
Mtayarishaji Simon Cowell (executive)
Steve Robson, Ryan Tedder, Carl Falk
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za Westlife
Back Home
(2007)
Where We Are
(2009)


Single ya kwanza kutoka katika albamu hii ilikuwa "What About Now" single ambayo ilitoka tarehe 23 Oktoba 2009.[9] single hii pia iliweza kutoka kama wimbo wa digitali na siku moja baadae kama ulitoka katika diski.[10]

Albamu hii ilifanikiwa kufika hadi nafasi ya 28 katika chati ya albamu za Uingereza na kufanikiwa kuuza nakala zaidi ya 427,000

Historia

hariri

Wimbo wa "Shadows" ambao ulikuwa umeshahakikiwa kujumuiishwa katika albamu hii, uliandikwa na Ryan Tedder akishirikiana na Alexander James McLean kwa ajili ya albamu ya saba ya kundi la Backstreet Boys iliyojulikana kwa jina la This Is Us lakini kwa bahati mbaya haukujumuishwa katika orodha ya nyimbo. Baadae ulikuja kununuliwa na studio za Simon Cowell kwa ajili ya albamu ya Leona Lewis ya Echo, lakini baadae ilikuja kuamuliwa kuwa wimbo huo ungependeza zaidi iwao ungeimbwa na kundi la wavulana na hivyo ukapewa kundi la Westlife .[11] Wimbo wa No More Heroes ulioandikwa na Lindy Robbins pia ulitarajiwa kutokezea katika albamu hii..[12].

Moja kati ya waimbaji wa kundi hili Feehily aliliambia gazeti la The Daily Mirror kuwa, "Tunataka albamu hii kuwa sehemu fulani hivi, kati ya mapenzi kutoka kwa mashabiki wetu, na mwelekeo ambao kundi letu linaelekea. Baada ya miaka 11, tunaona hii kama ngwe ya pili katika historia ya Westlilfe.."[13].

Filan akiongelea, maudhui ya albamu hii anasema kuwa,[14]

"Tukisema mwelekeo tofauti kidogo tunakuwa tunakosea, kwani bado tunaimba muziki wa pop, lakini kuna mabadiliko kidogo ndani yake, tumefanya kazi na watayarishaji tofauti ambao hatukuwahi kufanya nao kazi hapo kabla, na pia tumekuwa na watunzi wa nyimbo tofauti. Kuna nyimbo kumi na tatu katika albamu hii, na kati ya hizo nyimbi kumi na mbili ni za kwetu wenyewe, kwa hakika kuna aina tofauti tofauti ya nyimbo nyimbo, kwa ujumla hii ni albamu nzuri zaidi kuwahi kutengenezwa na kundi la Westlife.Mtiririko wa nyimbo na kila kitu ndani yake ni vya kusisimua, hata kama wewe sio shabiki wa Westlife lakini unapenda muziku, hakika utatambua ubora wa albamu hii..

Kuitangaza

hariri

Tarehe 25 Oktoba 2009, katika tamasha la The X Factor Westlife waliimba wimbo wa "What About Now". Tarehe 26 Oktoba waliimba wimbo huu katika televisheni ya GMTV na baadae kufanya mahojiano katika kipindi cha The One Show hii ikia ni tarehe 30 ya mwezi oktoba 2009 [15] Pia waliimba katika tamasha la BBC Children in Need tarehe 20 Novemba na tarehe 4 disemba waliimba katika vipindi vya Alan Carr's Chatty Man na kipindi cha The Friday Show .[15] Pia walifanya matangazo katika redio mbalimbali katika maeneo vituo mbalimbali vya redio vya Eire na Uingereza ikiwa ni pamoja na redio BBC Radio One [16] matamasha ya televisheni yalitangazwa baadae.[17][18] pia waliimba katika tamasha la nchini Uswidi katika mashindano ya Swedish Idol.[19] Tarehe 27 Novemba 2009, Westlife waliimba katika kipindi maarufu cha Uingereza cha Paul O' Grady Show na baadae kipindi cha The Late Late Toy Show.[20] Pia waliimba katika mji wa Oslo, nchini Norwei katika Tuzo za Nobeli za mwaka 2009.

Orodha ya nyimbo

hariri
# Wimbo M(Wa)tunzi M(Wa)tayarishaji Urefu
1. "What About Now" Ben Moody, David Hodges, Josh Hartzler Steve Robson 4:11
2. "How to Break a Heart" Sam Watters, James Scheffer, Louis Biancaniello Louis Biancaniello, Sam Watters, Jim Jonsin 4:04
3. "Leaving" Steven Lee Olsen, Bryn Christopher, Carl Falk Louis Biancaniello, Sam Watters (MzMeriq) 3:57
4. "Shadows" Ryan Tedder, Alexander James McLean[11] Ryan Tedder 4:01
5. "Talk Me Down" Simon Petty Steve Anderson 4:01
6. "Where We Are" Ryan Tedder, Savan Kotecha Ryan Tedder 3:57
7. "The Difference" Scott Cutler, Anne Preven, Brian Kennedy Seals Scott Cutler, Anne Preven, Brian Kennedy Seals (Team BK) 3:30
8. "As Love Is My Witness" Connor Reeves, Jonathan Shorten Martin Terefe 4:07
9. "Another World" Steve Booker, Sophie Delila Steve Booker 3:16
10. "No More Heroes" Lindy Robbins, Savan Kotecha, Emanuel Kiriakou[12] Emanuel Kiriakou 3:58
11. "Sound of a Broken Heart" Sam Watters, John Reid, Wayne Wilkins, Louis Biancaniello Louis Biancaniello, Sam Watters, Wayne Wilkins 3:51
12. "Reach Out" Chris Braide, Mark Feehily, Shaznay Lewis Greg Wells, Chris Braide 3:56
13. "I'll See You Again" Shelly Poole, Andy Hill Emanuel Kiriakou, Andy Hill 5:17
14. "You Raise Me Up (Live at Croke Park)"
(Japan Bonus Track)
Brendan Graham, Rolf Løvland Decca Records 5:00

Historia ya kutoka

hariri
Nchi / Eneo Tarehe Muundo Studio Catalogue
Eire 27 Novemba 2009 CD, MP3 RCA Records 88697611272
Ufilipino 28 Novemba 2009 Sony Music Entertainment
Nyuzilandi 30 Novemba 2009
Norwei[21]
Afrika Kusini[22]
Ufalme wa Muungano[23] Syco Music
Hong Kong[24] Sony Music Entertainment
Korea Kusini[25] 1 Desemba 2009
Ulaya[26] 2 Desemba 2009
Ufini[27]
Uswidi[28]
Japani[29] 23 Desemba 2009 Sony Music Japan SICP2509
Nchi Ilipata
nafasi
Mauzo Certification
Ufalme wa Muungano 2 600,000+ 2xPlatinum[30]
Eire 2 TBA TBA
Korea Kusini[31] 3 TBA TBA
Uswidi 8 20 000+ Gold
Nyuzilandi 13 TBA TBA

Marejeo

hariri
  1. BBC review
  2. "Entertainment Focus review". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  3. Daily Express review
  4. "Digital Spy review". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-16. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  5. "iAfrica review". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-09. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  6. "London Evening Standard review". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  7. "New! Magazine review". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-08. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  8. The Observer
  9. "What About Now: Westlife: Amazon.co.uk: MP3 Downloads". Amazon.co.uk. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
  10. "What About Now: Westlife: Amazon.co.uk: Music". Amazon.co.uk. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
  11. 11.0 11.1 "Music - News - Westlife 'given Leona Lewis song'". Digital Spy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-12-27. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
  12. 12.0 12.1 Robbins, Lindy. "UPDATED DISCOGRAPHY (10/04/09)". MySpace. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-07. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2009.
  13. "Westlife return with new single". mirror.co.uk. 2009-10-15. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
  14. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-26. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  15. 15.0 15.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-25. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  16. p://www.westlife.com/news/2009/10/29/westlife_on_the_radio_1
  17. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-15. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  18. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  19. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  20. "Tubridy thrilled with Toy Show figures". RTÉ Entertainment. 30 Novemba 2009. Iliwekwa mnamo 2 Desemba 2009.
  21. http://cdon.no/musikk/westlife/where_we_are-7544961
  22. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-04. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  23. "Where We Are: Westlife: Amazon.co.uk: Music". Amazon.co.uk. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
  24. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-29. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  25. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  26. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-16. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  27. http://cdon.fi/musiikki/westlife/where_we_are-7544961
  28. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-16. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  29. http://www.hmv.co.jp/en/product/detail/3703493
  30. "UK BPI searchable certification database". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-17. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  31. "South Korea Album Chart". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-29. Iliwekwa mnamo 2010-01-22.
  NODES
chat 4