"You Raise Me Up" ni wimbo maarufu wa kutia moyo. Wimbo huu uliandikwa na Secret Garden's Rolf Løvland na mashairi yaliandikwa na Brendan Graham, ambaye huyu alikua ni mwandishi maarufu wa nyimbo kutoka Jamuhuri ya Island. WImbo huu hadi sasa umekwisha kurudiwa zaidi ya mara 125 .[1] Wimbo huu kwa asili uliandikwa kama wimbo wa kuimbwa kwa vyombo pekee na ulikua ukijulikana kama Silent Story, na mahadhi ya wimbo huu yanaelekeana na yale ya tamaduni za Kiairish, hasa wakati wa kuanza kwa kiitikio. Løvland alimwendea mwandishi wa vitabu vya hadithi na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Irish Brendan Graham kuandika mashairi kwa ajili ya sauti zake za vyombo, hii ikiwa ni baada kusoma kitabu chake cha hadithi.[2] Wimbo huu ulitolewa kwa mara ya kwanza katika albamu ya Garden ya mwaka 2001 iliyokwenda kwa jila la Once in a Red Moon ikiwa na waimbaji kama vile Brian Kennedy, na kufanikiwa kupata mauzo mazuri nchini Ireland na Norway. Hapo awali, Brian Kennedy alitakiwa kufuatana na Secret Garden katika ziara yao ya mwaka 2002, lakini aliguua na hivyo kushindwa kuhudhuria. Na badala yake, nafasi yake ilichukuliwa na mwimbaji mwingine wa nchini Norway, aliyejulikana kwa jina la Jan Werner Danielsen, ambaye baadae pia alikuja kurekodi wimbo huo na Secret Garden lakini haukuwahi kutoka

"You Raise Me Up"
Inspirational wa Secret Garden
Urefu 5:04
Mtayarishaji Decca
Mwenendo
"You Raise Me Up"

Kurudiwa

hariri

Mwimbaji wa nchini Uingereza Becky Taylor aliurudia wimbo huu katika albamu yake ya pili iliyokwenda kwa jina la Shine iliitoka mnano 1 Julai 2003. Baadae pia, wimbo huu ulirekodiwa na Daniel O'Donnell mwaka 2003, na ulifanya vizuri nchini Ireland na Uingereza. Pia mwimbaji Tenor Javier Fontana alifanikiwa kurekodi wimbo huu. Baadae mwaka 2003, David Foster aliamua kuutengeneza tena wimbo huu ikiwa ni baada ya kupewa taarifa na mtayarishaji wa nyimbo aliyefahamika kwa jina la Frank Petrone wa Peermusic Alifanikiwa kutengeneza wimbo huo ambao ulionekana kufanya vizuri nchini Marekani na kufanikiwa kushika nafasi ya juu katika chati ya muziki ya Billboard na kufanikiwa kushika nafasi hiyo kwa wiki sita mfululizo Wimbo wa You Raise Me UP umekua ni wimbo uliofana vizuri zaidi kutoka kwa kundi la Westlife, hii ikiwa ni katika albamu yao ya tano iliyofahamika kwa jina la Face To Face. Wimbo huu ulifanikiwa kishika nafasi ya kwanza katika orodha ya nyimbo bora zaidi nchini Uingereza kwa mwaka 2005, na kuufanya kuwa wimbo wa kumi na tatu kutoka katika kundi hili kuweza kufika katika nafasi ya kwanza. Halikadhalika, wimbo huu umefanikiwa kuuza zaidi ya nakala 540,000 nchini Uingereza hadi sasa .[3]

Umaarufu

hariri

Kaitika mwaka 2004, wimbo huu ulikuwa ukipigwa zaidi ya mara 500,000 katika radio mbalimbali nchini Marekani. Baadae katika miaka ya 2005, wimbo huu ulikua umekwisha imbwa katika aina zaidi ya 80 tofauti tofauti, hii ikiwa ni kwa nchini Marekani peke yake. Wimbo huu ulishawai kutuliwa katika mashindano mbalimbali ya nyimbo za dini katika Wimbo bora wa mwaka. Tarehe 3 Desemba 2010, wimbo huu uliokua ukiimbwa na Josh Groban, uliimbwa mwishoni mwa michuano ya mpira ya Chuo Kikuu cha Michigan. Wimbo huu uliweza kuibua hisia, ambapo uliimbwa wakati wachezaji wakiwa wameshikana mikono ikiwa juu, na mwisho kocha wa timu ya mpira alionekana akifuta machozi kabla ya kutoa nasaha za mwisho

Toleo la Westlife

hariri
“You Raise Me Up”
Single ya Westlife
Muundo CD Single
Aina Pop
Urefu 4:01
Mtayarishaji Steve Mac

Orodha ya nyimbo

hariri
  • United Kingdom
CD1
  1. "You Raise Me Up" – 4:00
  2. "World Of Our Own" (Acoustic Version) – 3:30
CD2
  1. "You Raise Me Up" – 4:00
  2. "Flying Without Wings" (Acoustic Version) – 3:30
  3. "My Love" (Acoustic Version) – 3:48
  • Australia
  1. "You Raise Me Up" - 4:00
  2. "You Raise Me Up" (Chameleon Remix) - 3:17
  3. "You Raise Me Up" (Reactor Remix) - 3:29
Chart (2005) Peak
position
Australian Singles Chart 3
Austrian Singles Chart 59
Dutch Singles Chart 47
German Singles Chart 11
Irish Singles Chart 1
Norwegian Singles Chart 3
Swedish Singles Chart 7
Swiss Singles Chart 18
UK Singles Chart 1

Chati ya mwisho wa mwaka

hariri
End of year chart (2005) Position
Irish Singles Chart 1
UK Singles Chart 9
End of year chart (2006) Position
Australian Singles Chart 14[4]


  1. http://www.peermusic.com/peermusic/index.cfm/artist-writer/artist-details/?artist_id=351 Ilihifadhiwa 27 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine., paragraph 5
  2. "Lyrics by Secret Garden". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-17. Iliwekwa mnamo 2011-12-06.
  3. http://www.mtv.co.uk/music/charts/official-uk-countdowns/westlife-official-top-20
  4. http://www.aria.com.au/pages/ARIACharts-EndofYearCharts-Top100Singles2006.htm
  NODES
chat 5
inspiration 1