Yuda Iskarioti
Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), Myahudi wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16).
Mitume wa Yesu |
---|
|
Ni tofauti na mtume mwenzake Yuda Tadei.
Majina
haririKwa Kigiriki, katika Agano Jipya anaitwa Ιουδας Ισκαριωθ (Ioudas Iskariôth) na Ισκαριωτης (Iskariôtês).
Kwa kuwa Yuda ni jina la babu wa kabila kubwa la Israeli lililobaki baada ya yale ya Kaskazini kupotea uhamishoni (722 KK), lilitumiwa sana na Wayahudi, hata wawili kati ya mitume hao wanaitwa hivyo.
Ndiyo sababu ilibidi kuwatofautisha kwa jina la pili, ambalo kwake ni "Iskarioti", maana yake "mtu wa Kariot" (Ish Kariot) kutokana na kijiji cha asili (Keriot-Chezron kinachotajwa tu katika Kitabu cha Yoshua 15:25, kikiwa Kusini kwa Yudea, mipakani kwa Edomu, kwenye Neghev.
Tafsiri nyingine inategemea jina Ekariot ("gaidi") walilopewa wapiganiauhuru wakali zaidi, waliokuwa tayari kuua wakoloni popote pale.
Tafsiri ya tatu inazingatia neno la Kiaramu sheqarya' au shiqrai, linalomaanisha mtu dhalimu; "tapeli" linaweza kutafsriwa ishqaraya.
Tafsiri ya mwisho inategemea neno lingine la lugha hiyo, sakar, yaani anayekabidhi.
Katika Agano Jipya
haririYuda anatajwa katika Injili na mwanzoni mwa Matendo ya Mitume.
Humo tunasoma kwamba alikuwa mwekahazina wa kundi la Mitume (Injili ya Yohane 12:6) mwenye tabia ya udokozi ambaye hatimaye alimuuza Yesu Kristo kwa maadui wake wa Baraza la Israeli (Injili ya Mathayo 26:47-49).
Mapema baada ya tukio hilo alikufa vibaya (30 B.K.) na nafasi yake ikashikwa na Mtume Mathia.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yuda Iskarioti kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |