Zauditu wa Ethiopia

(Elekezwa kutoka Zauditu)

Zauditu (29 Aprili 18762 Aprili 1930) alikuwa malkia mtawala wa Uhabeshi kuanzia 27 Septemba 1916 hadi kifo chake. Alimfuata Iyasu V. Jina lake la kubatizwa lilikuwa Askala Maryam. Alikuwa mtoto wa kwanza wa Menelik II.

Malkia Zauditu wa Ethiopia

Mwanzoni utawala wake ulisumbuliwa na uasi wa Iyasu aliyekuwa ameuzuliwa. Malkia huyu anajulikana kwa jinsi alivyopenda dini na alivyokuwa mpinzani mkubwa wa mabadiliko aliyokuwa akiyafanya Ras Tafari Makonnen. Zauditu aligombana sana naye kuhusu mambo ya siasa lakini alishindwa. Naye Tafari alimfuata kama mfalme kwa jina la Haile Selassie.

Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zauditu wa Ethiopia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES