Abraham Lincoln

Rais wa 16 wa Marekani

Abraham Lincoln (12 Februari 180915 Aprili 1865) alikuwa Rais wa 16 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1861 hadi 1865.

Abraham Lincoln


Muda wa Utawala
Machi 4, 1861 – Aprili 15, 1865
Makamu wa Rais Hannibal Hamlin (1861–1865)
Andrew Johnson (Machi–Apr. 1865)
mtangulizi James Buchanan
aliyemfuata Andrew Johnson

tarehe ya kuzaliwa (1809-02-12)Februari 12, 1809
Kentucky, Marekani
tarehe ya kufa 15 Aprili 1865 (umri 56)
Washington, D.C., Marekani
mahali pa kuzikiwa Lincoln Tomb
chama Whig (Kabla ya 1854)
Republican (1854–1864)
National Union (1864–1865)
ndoa Mary Todd Lincoln (m. 1842) «start: (1842-11-04)»"Marriage: Mary Todd Lincoln to Abraham Lincoln" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Abraham_Lincoln)
watoto Robert Todd Lincoln
Edward Baker Lincoln
William Wallace Lincoln
Tad Lincoln
signature
Uuaji wa Lincoln.

Alikuwa na Kaimu Rais wawili: kwanza Hannibal Hamlin, halafu Andrew Johnson aliyemfuata kama Rais, Lincoln alipouawa.

Lincoln amejulikana kama rais wa upande wa kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani kati ya majimbo ya kaskazini dhidi ya Shirikisho la Madola ya Amerika la kusini.

Kwa hiyo hukumbukwa kama rais aliyeleta mwisho wa utumwa, yaani uhuru kwa watumwa wote wa Marekani na kuunganisha taifa tena.

Juhudi zake zilimgharimu uhai.

Lincoln na kufutwa kwa utumwa

hariri

Lincoln aliingia katika siasa alipokuwa wakili huko Springfield, Illinois; mwaka 1846 alichaguliwa mbunge wa kitaifa katika Nyumba ya Wawakilishi kwa kipindi kimoja. Mwaka 1849 alirudi kwa familia yake na kazi ya uwakili. Mwaka 1856 aliingia tena kwenye siasa alipoona upanuzi wa nguvu ya watetezi wa utumwa katika majimbo ya kusini ya Marekani. Aliunda tawi la Illinois ya Republican Party akateuliwa kuwa mgombea wa urais akachaguliwa rais wa Marekani kwenye Desemba 1860.

Lincoln alipinga utumwa lakini kwa asili hakuwa mpinzani mkali; aliona kwamba utumwa uliwahi kukubaliwa katika katiba ya Marekani tangu mwanzo lakini aliona hali hiyo iendelee katika majimbo ya kusini tu yaliyokuwa sehemu za Marekani tangu mwanzo ilhali majimbo ya kaskazini yaliukataa. Alipinga upanuzi wa utumwa katika majimbo mapya yaliyoendelea kuundwa wakati Muungano wa Madola ya Amerika ulipanua eneo lake upande wa magharibi na kuelekea utawala juu ya nchi yote kati ya Kanada na Meksiko.

Alipinga hatua ya majimbo ya kusini kujitenga na baada ya mashambulio dhidi ya vituo vya kijeshi vya Muungano aliamua kuchukua hatua za kijeshi ili kurudisha majimbo yaliyoasi. Mwanzoni mwa vita alitangaza nia yake haikuwa kumaliza utumwa kusini; lakini baada ya vita kuendelea miaka miwili alikuwa tayari kuchuka hatua kali zaidi.

Mwaka 1862 alitia sahihi tangazo la Bunge la Muungano kuwa watumwa wote waliomilikiwa na askari waliopiga vita dhidi ya Muungano wakamatwe na kutangazwa huru. Mwisho wa 1862 Lincoln mwenyewe alitoa amri ya kutangaza uhuru wa watumwa wote katika majimbo yote yaliyotumia silaha dhidi ya Muungano. Alikubali pia kuajiri watumwa kuwa wanajeshi kama wamekimbia kutoka upande wa kusini na kujitolea. Hakufuta kabisa utumwa kwa sababu bado kulikuwa na majimbo machache yenye utumwa yaliyobaki katika Muungano. Baada ya mwisho wa vita Lincoln alipata kibali cha bunge cha kufuta utumwa kabisa katika maeneo yote ya Marekani.

}}

  NODES