Afrika ya Kati ni kanda la bara la Afrika iliyoko katikati ya bara. Katika hesabu ya Umoja wa Mataifa (UM) nchi 9 zifuatazo huhesabiwa kuwa sehemu zake:

Jina la nchi au eneo,
bendera
Mji Mkuu
 
Angola
Luanda
 
Kamerun
Yaoundé
 
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Bangui
 
Chadi
N'Djamena
 
Kongo, Jamhuri ya
Brazzaville
 
Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia
Kinshasa
 
Guinea ya Ikweta
Malabo
 
Gabon
Libreville
 
São Tomé na Príncipe
São Tomé

Afrika ya Kati kwa maana ya mpangilio ya UM ni nchi kusini ya jangwa Sahara, mashariki ya Afrika ya Magharibi na upande wa magharibi wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Mto mkubwa wa kanda ni mto Kongo.

Mwisho wa ukoloni kati ya 1953-1963 palikuwa na Shirikisho la Afrika ya Kati la nchi za kisasa za Malawi, Zambia na Zimbabwe zinazohesabiwa siku hizi kuwa sehemu za Afrika ya Kusini au Afrika ya Magharibi.

  NODES