Agostino Cacciavillan

Agostino Cacciavillan (14 Agosti 19265 Machi 2022) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Italia na kardinali tangu mwaka 2001.

Alifanya kazi katika huduma za kidiplomasia za Vatikani kuanzia mwaka 1959 hadi 1998. Mnamo 1976, alipewa vyeo vya askofu mkuu na balozi wa kitume (nuncio), akihudumu kama Pro-Nuncio katika nchi za Kenya, India, Nepal, na Marekani hadi 1998.

Baadaye, alihudumu katika Curia ya Roma kama Rais wa Idara ya Utawala wa Mali za Kitume (Administration of the Patrimony of the Apostolic See) kuanzia 1998 hadi 2002. [1]

Marejeo

hariri
  1. Report on the Holy See's Institutional Knowledge and Decision-Making Related to Former Cardinal Theodore Edgar McCarrick (PDF). 10 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES
admin 1