Aït Benhaddou (kwa Kiberber: ⴰⵢⵜ ⴱⴻⵏⵃⴰⴷⴷⵓ; kwa Kiarabu: آيت بن حدّو) ni ksar au mji-ngome katika Moroko ya kusini. Zamani ilipitiwa na njia ya misafara baina ya maeneo ya jangwa la Sahara na mji wa Marrakesh.

Ait Benhaddou
Nyumba kubwa ya Ait Benhaddou

Ait Benhaddou iko takriban kilomita 100 upande wa kusini-magharibi wa Marrakesh kando ya mto wenye maji kwenye miezi ya mvua.

Wenyeji ni Waberber waliojenga makazi yao kwa namna ya ngome. Nyumba za familia huwa na ghorofa tatu au zaidi, zimejengwa kwa kutumia udongo ulioshindiliwa na kuwa tayari ya kuishi mle, kuhifadhi bidhaa na kujitetea dhidi ya mashambulio. Nyumba kubwa zilijengwa na wafanyabiashara walioshiriki katika misafara.

Katika karne ya 20 wenyeji walianza kutoka kwenye nyumba za kale na kujenga kijiji kipya kando ya makazi ya zamani. Lakini watalii wengi wanakuja kuangalia mfano huu wa ubunifu wa kihistoria uliopokewa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia tangu mwaka 1987.[1]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Ksar of Ait-Ben-Haddou kwenye tovuti ya UNESCO
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ait Benhaddou kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

  NODES