Akoliti (kwa Kiingereza "acolyte", kutoka Kigiriki ἀκόλουθος, akoluthos, yaani "msindikizaji") ni Mkristo anayemsaidia askofu, padri au shemasi anapoongoza ibada fulani[1].

Akoliti alivyochorwa na Abraham Solomon, 1842.
Akoliti wa Armenia akishika "ripida".
Akoliti wa Kanisa la Kilatini akimshikilia askofu kitabu cha ibada wakati wa kuweka wakfu altare.

Katika Kanisa la Kilatini

hariri

Katika Kanisa la Kilatini tangu mwaka 1972, pamoja na usomaji, ni mojawapo kati ya huduma mbili za lazima[2] ambazo wale wote wanaojiandaa kupata daraja takatifu wazipate na kuzitekeleza kwa muda fulani.

Kati ya kazi muhimu za akoliti, mojawapo ni kuwagawia waamini wenzake sakramenti ya ekaristi[3].

Kuanzia mwaka 2021 wanawake pia wanaweza kupewa kazi hiyo, baada ya Papa Fransisko kurekebisha kanuni 230 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa.

Tanbihi

hariri
  1. General Instruction of the Roman Missal
  2. "Ministeria quaedam, II".
  3. General Instruction of the Roman Missal, no. 100

Marejeo

hariri
  • John N. Wall. A Dictionary for Episcopalians. Cambridge, MA: Cowley Publications, 2000.
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akoliti kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 1