Arinabu (kwa Kilatini na Kiingereza Lepus) [1] ni jina la kundinyota lililopo upande wa kusini mwa ikweta ya anga

Nyota za kundinyota Arinabu (Lepus) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Arinabu - Lepus jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kusini

Mahali pake

Arinabu (Lepus) liko karibu na ikweta ya anga linapakana na makundinyota jirani ya Mbwa Mkubwa (Canis Major), Munukero ( Monoceros), Jabari (Orion), Nahari (Eridanus), Patasi (Caelum)' na Njiwa (Columba).

Jina

Arinabu (Lepus, kwa maana ya „sungura“) lilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الأرنب al-ʾarnab kwa maana ya “sungura” [2]. Waarabu walitafsiri hapa jina la Klaudio Ptolemaio aliyetaja nyota hizi vile kwa jina la Λαγωός lagôos katika orodha yake ya Almagesti [3]. Wagiriki walimwona hapa sungura anayekimbia mbele ya mwindaji Jabari (en:Orion)

Lepus - Arinabu ni kati ya makundinyota 48 yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [4] kwa jina la Lepus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Lep'.[5]

Nyota

Nyota angavu zaidi ni Alfa Leporis au Arneb [6]. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 2.58 ikiwa na umbali wake unaokadiriwa kati ya miakanuru 1,200 na 2,200 kutoka Dunia[7][8].

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α 11 Arneb 2,58m 1200 - 2200 F0 Ib
β 9 Nihal 2,81m 160 G5 II
μ 5 3,0 bis 3,4m 200 B9 III
ε 2 3,19m 150 K5 III
ζ 14 3,55m 70,5 A2 IV-V(n)
γ 13 3,59m 29,3 F6V + G5
η 16 3,72m 49,1 F2 V
δ 15 3,76m 150 G8 III
Habari za mwangaza na umbali vinaweza kubadilika kutokana na vipimo vipya

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Lepus" katika lugha ya Kilatini ni "Leporis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Leporis, n.k.
  2. ling. Knappert 1993
  3. PAL - Glossary "Lep", tovuti ya mradi wa "Ptolemaeus Arabus et Latinus (PAL)" wa Bavarian Academy of Sciences and Humanities, iliangaliwa Oktoba 2017
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  5. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
  6. Arneb - Naming Stars , tovuti ya Ukia, iliangaliwa Novemba 2017; hapa jinsi ilivyo pia kwa kundinyota nyingine jina rasmi la nyota angavu zaidi linatunza hapa jina la Kiarabu lililokuwa kawaida kwa kundinyota yote
  7. Lepus, tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  8. Arneb (Alpha Leporis), tovuti ya Prof. Jim Kaler

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 131 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331

Viungo vya Nje


  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Arinabu (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


  NODES
INTERN 2