Asunción ni mji mkuu wa Paraguay. Jiji lina wakazi milioni 1.6. Maana ya "asuncion" ni "kupalizwa (mbinguni)". Jina kamili kwa Kihispania ni "Nuestra Señora Santa María de la Asunción" (Mama yetu Mtakatifu Maria wa kupalizwa). Jina limechaguliwa kwa kukumbuka siku ya mji kuundwa na conquistador Juan de Salazar tarehe 15 Agosti 1537 ambayo ni sikukuu ya kupalizwa kwake Mariamu mbinguni katika kalenda ya liturujia ya Kilatini ya Kanisa Katoliki.

Asuncion, Paraguay


Jiji la Asunción
Nchi Paraguay
Mahali pa Asunscion katika Paraguay
Panteón de los Héroes mjini Asunción

Jiji ni kitovu cha uchumi, utamaduni na siasa ya nchi.

Asuncion ipo kando ya mto Paraguay ikitazama mdomo wa Río Pilcomayo upande wa Argentina.

Ni kati ya miji ya kwanza iliyoundwa na Wahispania katika Amerika Kusini. Kwa sababu hiyo huitwa mara nyingi "Mama wa miji".

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Asuncion kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  NODES