Bata mzinga
Bata mzinga kaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Galliformes (Ndege kama kuku)
Familia: Phasianidae (Ndege walio na mnasaba na kwale)
Nusufamilia: Meleagridinae (Ndege walio na mnasaba na bata mzinga)
Jenasi: Meleagris
Linnaeus, 1758
Spishi: M. gallopavo Linnaeus, 1758

M. ocellata Cuvier, 1820

Mabata mzinga au mapiru (kwa Kiingereza anaitwa turkey) ni ndege wakubwa wa jenasi Meleagris, jenasi pekee ya nusufamilia Meleagridinae katika familia Phasianidae. Ndege hawa ni wakubwa kabisa kati ya Phasianidae.

Yai la Meleagris gallopavo

Wanafanana kidogo na bata, wana manyoya ya kahawia,kichwa kisicho na manyoya na shingo yenye ngozi ya makunyazi isiyo na manyoya. Kichwa chao hakina manyoya na kina rangi nyekundu, pinki au ya kijivu. Manyoya yana rangi nyeusi imetayo yenye madoa.

Hula makokwa, mbegu, beri, mizizi na wadudu, pengine amfibia na watambaachi.

Jike hutaga mayai 10-14 huku wengine kufikia hadi idadi ya mayai 20, katika shimo la kina kifupi. Makinda hutoka tago katika masaa 12-24.

Spishi moja (M. gallopavo) hufugwa kila mahali pa dunia.

Spishi

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri
  • Meleagris californica (Mwisho wa Pleistocene ya Marekani ya kusi-magharibi)
  • Meleagris crassipes (Mwisho wa Pleistocene ya Marekani ya kusi-magharibi)
  • Meleagris sp. (Mwanzo wa Pliocene ya Bone Valley, MMA)
  • Meleagris sp. (Mwisho wa Pliocene ya Macasphalt Shell Pit, MMA)
  Makala hii kuhusu ndege fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bata Mzinga kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES