Billie Eilish Pirate Baird O'Connell [1] (alizaliwa Desemba 18, 2001) ni mwimbaji, na mtunzi wa nyimbo wa Marekani.

Billie Eilish
Billie Eilish, mnamo 2019
Billie Eilish, mnamo 2019
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Billie Eilish Pirate Baird O'Connell
Amezaliwa 18 Desemba 2001 (2001-12-18) (umri 23)
Aina ya muziki Pop
Kazi yake Mwimbaji
Ala Sauti
Miaka ya kazi 2015 - hadi leo
Studio Polydor Records
Tovuti billieeilish.com

Alipata umaarufu kwa mara ya kwanza mnamo 2015 na wimbo wake wa kwanza "Ocean Eyes", ulioandikwa na kutayarishwa na kaka yake Finneas O'Connell, ambaye anashirikiana naye kwenye muziki na matamasha ya moja kwa moja. Mnamo 2017, alitoa albamu yake ya kwanza, ulioitwa Don't Smile at Me. Mafanikio kibiashara, ilifikia 15 bora ya chati za rekodi katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza, Canada, na Australia.

Albamu ya kwanza ya Eilish ya studio, When We All Fall Asleep, Where Do We Go? (2019), ilianza juu ya Chati ya Albamu ya Billboard 200 ya Marekani na Uingereza. Ilikuwa moja ya albamu zilizouzwa zaidi mwaka huo (2019), ikichangiwa na mafanikio ya wimbo wake wa tano "Bad Guy", nambari moja ya kwanza ya Eilish kwenye Billboard Hot 100 ya Marekani. Hii ilimfanya kuwa msanii wa kwanza kuzaliwa katika karne ya 21 kutoa single iliyoshika chati. Na ndani ya mwaka alitoa nyimbo kadhaa ikiwemo "8" [2]mwezi wa nne 2019 ilioshika nafasi ya 79 kwenye Billboard Hot 100. Mwaka uliofuata, Eilish aliimba wimbo wa "No Time to Die" kwa filamu ya James Bond ya jina moja, ambayo iliongoza chati ya Uingereza Singles Chart na kushinda Tuzo ya Academy ya Wimbo Bora wa Asili mnamo 2022(Academy Award for Best Original Song). Nyimbo zake zilizofuata "Everything I Wanted", "My Future", "Therefore I am", na "Your Power" zilishika nafasi ya 10 bora nchini Marekani na Uingereza. Albamu yake ya pili ya studio, "Happier Than Ever" (2021), iliongoza chati katika nchi 25.

Marejeo

hariri
  1. "Billie Eilish: Is she pop's best new hope?", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2017-07-15, iliwekwa mnamo 2022-12-13
  2. "List of songs recorded by Billie Eilish", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-11-05, iliwekwa mnamo 2022-12-13
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Billie Eilish kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
chat 5