Bridgetown ni mji mkuu wa Barbados ambayo ni nchi ya visiwani ya Karibi kati ya visiwa vya Antili Ndogo. Bridgetown ni mji mdogo tu mwenye wakazi 7,000 lakini pamoja na watu wa eneo la karibu ni mnamo 90,000. Uko kwenye pwani la kusini-magharibi ya kisiwa cha Barbados.

Bridgetown

Kitovu cha Bridgetown pamoja na bandari yake
Habari za kimsingi
Utawala sehemu ya ushirika raia wa St. Michael (parish of Saint Michael)
Anwani ya kijiografia Latitudo: 13°7′N - Longitudo: 59°37′W,
Kimo takr. 3 - 52 m juu ya UB
Eneo - Ushirika raia 39 km²
- mji ? km²
Wakazi watu 7,000 mjini
takriban 90,000 katika rundiko la mji (2006)
Msongamano wa watu watu 2,303 kwa km² (ushirika)
Simu + 1 246 (nchi yote)
Mahali

Mji ulianzishwa na Waingereza mnmo 1628 kando la mdomo wa Constitution River. Mdomo huu unaoitwa "Careenage" ni pia bandari kwa jahazi ndogo za watalii.

Kuna nyumba kadhaa zilizojengwa wakati wa ukoloni wa Uingereza kama vile Bunge, kanisa la St. Micheal's, Harrison College na mengine.

Uchumi umetegemea siku hizi hasa utalii. Mashamba ya miwa yameendelea na bidhaaa kutokana na miwa ni sukari na pombe aina ya Rum.

Kila mwezi wa Januari kuna sherehe ya musiki ya Barbados Jazz Festival mjini Bridgetown.

  NODES