Buganda ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Mfalme wa Buganda anatumia cheo cha Kabaka. Jina la nchi Uganda ni umbo la Kiswahili la neno Buganda.

Bendera ya Buganda.
Eneo la Buganda kati ya ziwa Viktoria, mto Nile na ziwa Kyoga.

Tangu karne ya 18 BK hadi karne ya 20 Buganda ilikuwa dola lenye enzi katika eneo la Ziwa Viktoria.

Leo hii ni sehemu ya Uganda yenye madaraka ya kiutamaduni pamoja na kuwa na bunge lake, lakini si kitengo cha kiutawala ndani ya Uganda.

Eneo na watu

hariri

Eneo la Buganda liko kaskazini na magharibi kwa Ziwa Viktoria hadi mto Nile upande wa mashariki na ziwa Kyoga kaskazini.

Watu wake huitwa Waganda (kwa Kiganda: "Baganda") wanotumia lugha ya Kibantu. Wako takriban milioni tatu ambao ni kabila kubwa la Uganda lenye 16.7% ya wakazi wote wa nchi. Kuna koo 52 kati ya Waganda.

Makaburi ya kihistoria ya wafalme wa Buganda huko Kasubi (Kampala) imeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.

Historia

hariri

Mwisho wa karne ya 19 Buganda ilikuwa lengo la majaribio ya nchi mbalimbali ya nje ambazo zilitaka kuwa na athari hapa. Wamisionari Wakatoliki kutoka Ufaransa na Waanglikana kutoka Uingereza walishindana na Waislamu kwenye ikulu ya Kabaka Mutesa I (18561884) kati yao na dhidi ya wafuasi wa dini za jadi. Mashindano hayo yalisababisha kutokea kwa vyama mbalimbali vilivyoleta nchi katika hali ya vurugu.

Mnamo 1890 Mjerumani Karl Peters alifaulu kupata mkataba wa ushirikiano na Kabaka lakini serikali za Ujerumani na Uingereza zilipatana katika mkataba wa Helgoland-Zanzibar nchi iwe eneo la athari ya Uingereza. Mwakilishi Mwingereza Frederick Lugard aliingilia kijeshi kati ya mapigano ya vikundi ndani ya Buganda na kuhakikisha utawala wa Kabaka Mwanga II aliyehesabiwa kuwa upande wa Waanglikana, hivyo karibu na Uingereza. Mwaka 1894 Kabaka alikubali mkataba wa ushirikiano na Uingereza ambao machoni mwake ulikuwa mapatano ya hiari lakini hali halisi Buganda ikawa Nchi lindwa chini ya Uingereza.

Polepole utawala wa Kiingereza ilibadilisha hali ya Buganda hadi kuwa sehemu tu ya Uganda yote.

Wakati wa uhuru Waganda walishindwa kupata hali ya ufalme kuwa sehemu ya nchi inayojitawala lakini Kabaka Sir Edward Mutesa II alikuwa Rais wa Taifa pamoja na waziri mkuu Milton Obote.

Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini. Kwa muda wa miaka 30 ufalme wa Buganda ulifutwa kisheria. Kabaka Edward Mutesa II alikufa ng'ambo Uingereza.

Mwaka 1986 serikali mpya ya Yoweri Museveni ilimkaribisha Ronald Muwenda Mutebi, mtoto wa Kabaka marehemu, arudi Kampala. Baada ya Bunge la Uganda kurudisha falme za kihistoria ndani ya Uganda za Banyoro, Ankole na Toro pamoja na Buganda, Mutebi alifanywa Kabaka mpya mwaka 1993.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Buganda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES