Caracas (tamka: karakas) ni mji mkuu wa Venezuela. Mji uko katika kaskazini ya nchi karibu na bahari ya Karibi katika kimo cha 920 m juu ya UB. Idadi ya wakazi ni kati ya milioni 3 au 4.

Jiji la Caracas
Nchi Venezuela

Mji uliundwa na Mhispania Diego de Losada tar. 25 Julai 1567 kwenye mahali pa kijiji cha Kiindio cha Catuchacao kwa jina la Santiago de León de Carácas.

Mji ulikua tangu 1750 kutokana na kilimo na biashara ya kakao.

Baada ya uhuru wa Venezuela mwaka 1831 ilikuwa mji mkuu wa jamhuri mpya.

Idadi ya wakazi ilikua polepole katika karne ya 19 hadi kufikia takriban 90,000 mnamo 1900.

Baada ya kupatikana kwa mafuta ya petroli nchini uchumi ulipanuka na kuvuta wakazi wengi wapya.

Kati ya wenyeji wa Caracas ni Francisco de Miranda (*1750) na Simon Bolívar (*1783) waliozaliwa wote mjini.

Mitaa ya vibanda inapatikana kwenye mitelemko wa milima
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Caracas kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1
see 1