Cesc Fabregas

Mchezaji wa soka wa nchini Hispania

Francesc "Cesc" Fabregas Soler, ni mchezaji wa soka anayetokea nchini Hispania; alizaliwa tarehe 4 Mei 1987 katika mji wa Arenys De Mar. Anacheza kama kiungo wa kati katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea na timu ya taifa ya Hispania.

Cesc Fàbregas akiwa Arsenal, Agosti 2007.
Cesc Fabregas akiwa na klabu yake ya sasa ya Chelsea (2015)

Fabregas alikuzwa kipaji na chuo cha La Masia kwa vijana wa Barcelona F.C.. Aliacha akademi hiyo akiwa na miaka 16 na kusajiliwa na klabu ya Premier League ya Arsenal mnamo Septemba 2003. Baada ya viungo wa timu hiyo kupata majeraha alipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika msimu wa 2004-2005 na alifanikiwa kuzuia mipango ya timu pinzani na kuibuka mchezaji bora katika nafasi yake na kushinda kombe la FA mwaka 2005.

Akiwa na miaka 24 alisaini mkataba na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal mnamo septemba 2007.

Baada ya hapo alihamishwa na kurudishwa tena Barcelona kwa £35 kutoka London 15 Agosti 2011. Kwa miaka mitatu aliyokaa Camp Nou alicheza pembeni ya Xavi na Iniesta na kufanikiwa kushinda mataji kama La liga, Klabu Bingwa ya Dunia, Copa Del Rey, UEFA Super Cup na Spanish Super Cup.

Mnamo Juni 2014 alirudi tena London kwa wapinzani wa Arsenal Chelsea kwa ada ya £ milioni 30, na mwaka wake wa kwanza huko Chelsea alisaidia kupata ushindi wa Ligi Kuu.

Anachezea Premier League kwa sasa klabu ya Chelsea nafasi ya kiungo wa kati na timu ya taifa ya Hispania.

Cesc Fabregas akiwa na klabu yake ya zamani ya Arsenal akikabwa na Younes Kaboul (2010)

Katika ngazi ya timu ya taifa Fabregas alianza kucheza mwaka 2006 na kuiwakilisha nchi yake kwenye FIFA World Cup 2006, UEFA Euro 2008, 2009 FIFA Confederations Cup, 2010 World Cup, Euro 2012, Confederations Cup 2013, World Cup 2014 na Euro 2016.

Kwenye mashindano ya European Championship Fabregas aling'ara sana na kuwa chanzo cha ushindi 2008 na 2012 na mwaka 2010 ndiye aliyetoa pasi kwa Andres Iniesta iliyozaa goli kwenye fainali ya kombe la dunia alipata kepu yake ya 100.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cesc Fabregas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1