Chandigarh ni mji wa Uhindi kaskazini. Eneo lake lahesabiwa kama eneo maalumu la kitaifa, si sehemu ya jimbo lolote, lakini wakati huohuo ni mji mkuu wa majimbo mawili jirani, yaani Punjab na Haryana.

Ikulu ya Bunge Chandigarh
Mahali pa Chandigarh katika Uhindi

Eneo lina kilomita za mraba 114 na idadi ya wakazi inafikia milioni 1.1.

Lugha kuu ni Kipunjabi, Kihindi na Kiingereza.

Hadi mwaka 1947 Chandighar ilikuwa kijiji cha kawaida. Baada ya ugawaji wa Punjab kati ya Uhindi na Pakistan iliteuliwa kama mahali opa mji mkuu mpya upande wa Kihindi. Kundi la wasanifu wa kimataifa lilipanga mji mpya na mashuhuri kati yao alikuwa Mswisi Le Corbusier.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chandigarh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1