Divina Commedia (yaani "Tamthilia ya Kimungu") ndiyo jina la Kiitalia la kazi kuu ya Dante Alighieri (14 Mei/13 Juni 1265 - 13/14 Septemba 1321), iliyomfanya ahesabiwe mshairi bora wa lugha hiyo, tena mshairi muhimu zaidi wa kipindi cha zama za kati za Ulaya.

Dante Alighieri jinsi alivyochorwa na Giotto wakati wa maisha yake.

Muundo

hariri

Ni shairi refu ambamo anatoa habari za safari yake ya kidhahania huko ahera akipitia jehanamu, toharani hadi paradiso. Ndiyo sehemu tatu za shairi hilo zinazomwezesha kukiri imani yake ya Kikristo na kuchukua msimamo kuhusu watu na matukio hasa ya wakati wake.

  NODES
os 1