Edmundi Campion, S.J. (London, 24 Januari, 1540Tyburn, 1 Desemba 1581) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza, maarufu kwa akili na imara katika imani.

Mt. Edmundi alivyochorwa.

Ujanani alikubali kuwa Mwanglikana na kupewa ushemasi katika ushirika huo, lakini alijuta mapema na kukiri tena imani sahihi huko Ireland.

Baada ya kuhama Funguvisiwa la Britania, alijiunga na Wajesuiti huko Roma akapewa upadrisho huko Praha, Ucheki.

Mwaka 1580 alitumwa kwao alipojitahidi kuimarisha Wakatoliki kwa maneno na maandishi.

Mwaka uliofuata, akiwa anasoma Misa kwa siri alikamatwa na hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande[1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu na Papa Paulo VI mwaka 1976.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Desemba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri

The most comprehensive and detailed scholarly reference today is Professor Gerard Kilroy's biography: Edmund Campion, A Scholarly Life London & New York: Routledge "Ashgate", 2015. ISBN 978-1-4094-0151-3

Vyanzo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES
Project 2