Enduro ni aina ya mashindano ya pikipiki unaofanyika kwenye maeneo yasiyo na barabara maalumu au kwenye barabara za vumbi.[1] Enduro ni mchezo wenye vikwazo na changamoto nyingi kwenye eneo na barabara za kuchezea.

Mshini wa dunia mara nne Stefan Merriman akiendesha pikipiki kutoka kampuni ya Yamaha

Aina kuu ya mashindano ya Enduro ni yale ya mashindano ya Dunia ambapo mfumo wa mashindano hayo huangalia zaidi muda. Washiriki hushindana kwa kujaribu kumaliza mizunguko au vituo vilivyowekwa kwa kutumia muda mfupi zaidi.

Enduro za Kufuata Muda

hariri
 
Muendeshaji wa pikipiki aina ya KTM kwenye mashindano ya de Dinant Enduro mwaka 2007

Katika mashindano yaliyozoeleka ya Enduro ya kufuata muda, waendeshaji huondoka pamoja kwa makundi au safu, na kila safu huanza kwa dakika fulani. [1] Lengo la tukio ni kufika katika vituo vya ukaguzi vilivyowekwa kwa ratiba maalum. [1] Kuwasili mapema au kuchelewa husababisha alama za waendeshaji kupunguzwa. [1] Katika siku nzima, kutakuwa na vipindi vilivyotengwa kwa ajili ya kujaza mafuta na kuhudumia mashine. Adhabu hutolewa kwa kutokufuata muda uliowekwa au kwa kupokea msaada wa nje pale usiporuhusiwa. [2]

Enduro na Rally

hariri
 
Pikipiki aina ya E2 ikiruka kikwazo Arratzu, Spain.

Kuna aina mbili tofauti ya matukio – Enduro na Rally. Katika ya jamii ya kimataifa ya waendesha pikipiki za nje ya barabara, neno enduro kihistoria linaashiria hasa matukio ya kuangalia muda yanayohitaji washiriki kudumisha wastani fulani wa mwendo wa maili kwa saa kwenye eneo lenye ardhi tofauti. Washiriki husimamiwa kupitia mfululizo wa vituo vya siri vya kuangalia muda kando ya njia ya mashindano, na hupokea adhabu kulingana na wakati wa kufika katika vituo hivyo. [3][4] Rally, kwa upande mwingine, zinafanyika katika barabara yenye vituo kutoka sehemu moja hadi nyingine ambapo mshiriki mwenye muda wa kasi zaidi kati ya vitu hutangazwa mshindi. Njia hizo zinaweza kuwa fupi kuliko urefu wa jumla wa mbio, na katika hali hiyo, njia hurudiwa mara kadhaa, kila rudio likiitwa mzunguko. Njia hizo pia zinaweza kuwa ndefu sana kiasi kwamba washiriki hawapiti sehemu moja mara mbili. Nchini Marekani, muundo wa rally umeongezeka umaarufu na mara nyingi huitwa "Enduro". Mfululizo wa mashindano yaAMA imekuwa ikitumia muundo wa aina hiyo tangu mwaka 2007, uliopea jina la "start-control / restart enduros". Muundo huu unadhaniwa kuwa rahisi zaidi kwa waendeshaji wapya kwa kupunguza ugumu wa muundo wa mbio pamoja na kufanya alama kuwa rahisi kwa waandaaji. [5] Rally na Enduro zina sifa mbili kuu zilizoshabihiana; mara nyingi mashindano huwa ni marefu ikilinganishwa na aina nyingi za mbio za magari au pikipiki na hufanyika kwenye ardhi tofauti ya nje ya barabara, mara nyingi bila kurudia sehemu yoyote ya ardhi hiyo wakati wa tukio. Mifano ya rally hizo ni pamoja na Baja 500 na Baja 1000, zinazotangazwa na kusimamiwa na SCORE International na ni kati ya mbio maarufu za nje ya barabara za umbali mrefu. Mbio za nje ya barabara zinazochukua siku kadhaa na zinazojumuisha aina tofauti za hatua, baadhi zikiwa za kupimwa muda na nyingine zisizopimwa, kwa kawaida huitwa rally (neno linalotumika sana nchini Uingereza ambalo lina maana sawa na rally ya nje ya barabara) kama vile Dakar Rally.

Pikipiki

hariri
 
Pikipiki daraja E2 maalum kwa mashindano ya Dunia ya Enduro.

Pikipiki ya enduro huwa na muundo maalumu ili kuhumili asili ya michezo hiyo, ikiwa na suspension maalumu kwa ajili ya pikipiki za mashindano pamoja na sifa za kuifanya iweze kupita kwenye barabara za uma ambazo hu ani sehemu ya njia za kuchezea. Injini kwa kawaida ni za silinda moja kati ya CC 125 na 3003, au kati ya 250 na CC 6503 . Mnamo mwaka 1973, Yamaha ilitamblisha pikipiki maalumu kwa matumizi ya njia za milimani ambayo ilikuwa na neno enduro kama alama kwenye paneli za upande. Michuano ya dunia ya Enduro pamoja na michuano mingine, hugawanya pikipiki za enduro katika madaraja matatu; Enduro 1 (cc 100–125 au cc 175–250), Enduro 2 (cc 175–250 au cc 290–450) na Enduro 3 (cc 290–500 au cc 475–650).

Matukio

hariri
 
Samuli Aro akiendesha pikipiki aina ya KTM katika michuano ya dunia.

Matukio makubwa kwenye kalenda ya enduro ni pamoja na World Enduro Championship (WEC), International Six Days Enduro (ISDE), na mashindano kadhaa ya kitaifa. Chombo kinachosimamia enduro duniani ni Fédération Internationale de Motocyclisme (FIM). Kwa nchini Marekani, chombo kinachosimamia ni American Motorcycle Association (AMA). Nchini Uingereza, chombo kinachosimamia ni Auto-Cycle Union.

Mashindano ya Dunia ya Enduro

hariri

World Enduro Championship (WEC) ilianzishwa mwaka 1990, ikichukua nafasi ya European Enduro Championship, ambayo ilikuwa ikifanyika tangu 1968. Mashindano haya yanaendeshwa chini ya FIM na kwa kawaida yanajumuisha karibu Grands Prix nane au tisa kote duniani. Matukio haya hugawanywa katika siku mbili (na mbio mbili tofauti), ambapo pointi kuelekea ubingwa wa dunia hutolewa. Kila raundi inajumuisha motocross test na "extreme test," mbali na enduro test. Katika mashindano ya Dunia ya Enduro mwaka 2008, Mika Ahola wa kampuni ya Honda alishinda daraja 1 la Enduro, Johnny Aubert kutoka Yamaha alichukua daraja la 2, na Samuli Aro wa KTM alishinda taji lake la tano daraja la 3.

Mfululizo wa Mashindano ya Dunia ya Enduro

hariri

World Enduro Super Series (WESS) ni mashindano yaliyoanzishwa mwaka 2018. Mbio zote katika mfululizo huu zilikuwa zikiendeshwa kama matukio tofauti awali, na mfululizo huu unajumuisha mbio 11 kutoka Ulaya nzima ili kumpata Bingwa wa Dunia wa Enduro. Waendeshaji bora wa enduro kutoka duniani kote huja kushindana kwenye “hare scrambles, hard enduros, na enduro cross”,[clarification needed] enduro za jadi, nk. Red Bull huonyesha mubashara mfululizo michezo yote kwenye chaneli ya youtube, na tovuti ya WESS husasisha kalenda ya ratiba ya matukio kila mwaka.

International Six Days Enduro (ISDE) imekuwa ikifanyika tangu 1913, na ni tukio la zamani zaidi la michezo ya nje ya barabara kwenye kalenda ya FIM. Tukio hili huwaleta pamoja waendeshaji bora kuwakilisha timu zao za kitaifa, na mara nyingi huitwa "Kombe la Dunia la Enduro" au "Michezo ya Olimpiki ya Pikipiki".

American Motorcycle Association ni chombo kikuu kinachosimamia mashindano ya pikipiki za aina yote nchini Marekani. Mfululizo wa AMA mara nyingi unafanana na mfululizo wa FIM. East Coast Enduro Association ni mojawapo ya waandaaji mashuhuri wa mbio za enduro nchini Marekani. ECEA ina madaraja mbalimbali yaliyogawanywa kwa aina za pikipiki na demografia ya waendeshaji ambayo huruhusu mwendeshaji mwenye sifa kuchagua daraja la kushindana. Kila daraja la ujuzi (A, B, C) linagawanywa katika madaraja madogo kulingana na aina ya mashine, umri wa mwendeshaji, na jinsia. Mifano ni pamoja na "C 4-stroke," "C-Veteran (30+)," "B 2-Stroke Light," "B 2-Stroke Heavy," "Women's," nk. Kwa ujumla, zawadi hutolewa katika ngazi ya tukio na msimu kwa kila daraja dogo (kwa mfano, "Nilikuwa mshindi wa B 2-Stroke Light kwenye tukio hili..."). Madaraja yanajumuisha vikundi vya umri hadi 80+ (daraja la Legends). Ifuatayo ni orodha ya madaraja ya pikipiki: • Daraja AA - Ngazi ya juu zaidi ya mwendeshaji, sawa na "Class A," lakini wanaoshindania pointi kama sehemu ya AMA National Enduro Championship. Kwa mfano, Mike Lafferty, ambaye ni bingwa wa kitaifa wa AMA mara saba, hushindana katika daraja la AA. • Daraja A - Hawa pia ni waendeshaji wa kasi, lakini hawashindani kwa pointi kama sehemu ya ubingwa wa kitaifa. Zawadi zao zinahusiana na Ukanda wa AMA wanaposhindana. Ni washiriki wa ridhaa, ingawa wana ujuzi sawa na wengi wa waendeshaji wa AA. • Daraja B - Hii ni ngazi ya pili ya ujuzi wa mwendeshaji (hatua moja juu ya ngazi ya awali ya C-class). Waendeshaji "hupandishwa daraja" na AMA wanapopata idadi fulani ya pointi (pointi za kupandisha daraja ni tofauti na pointi zinazotolewa wakati wa mbio; pointi wakati wa mbio ni mbaya, kwani lengo ni kumaliza tukio ukiwa na pointi inayokaribia 0 kadiri uwezavyo, wakati pointi za kupandishwa daraja hutolewa mwishoni mwa kila tukio kulingana na jinsi mwendeshaji alivyofanya - matumizi mawili ya neno "pointi" mara nyingi huchanganya kwa waangalizi wa nje, kwa sababu maana ya kuwa na pointi wakati wa tukio ni hasi, wakati maana ya kuwa na pointi kuhusiana na msimamo wa mwendeshaji katika mfululizo ni chanya kwa ujumla). • Daraja C - Hii ni ngazi ya mwanzo ambapo waendeshaji wote wapya huanza. Waendeshaji wote huanza kama C-class riders na ikiwa wataendelea kushiriki na kumaliza matukio wataweza kupandishwa daraja hadi B-class baada ya misimu miwili au mitatu. Waendeshaji wa kipekee watapanda hadi B-class baada ya msimu wao wa kwanza kwa sababu watakuwa wamekusanya pointi zinazohitajika kwa haraka.

Matukio ya Kikanda

hariri

Mbali na mbio na mfululizo unaoidhinishwa na mashirika ya kitaifa, matukio mengi pia hufanyika katika ngazi ya ndani na kikanda na mashirika madogo yanayosimamia. Nchini Marekani, matukio haya yanafanana sana na yale yaliyoidhinishwa na AMA, yakitumia madaraja ya ujuzi ya A, B, C. Waendeshaji wengi huanza kazi zao za mbio kwenye matukio kama haya.

Umaarufu

hariri
 
Watazamaji wakimuangalia mchezaji wa daraja la vijana nchini Italia.

Umaarufu wa enduro hutofautiana sana kulingana na bara, nchi, ukanda, na hata aina ya tukio. Matukio mengine maarufu mara nyingi huainishwa kama enduros ingawa hufaa zaidi katika kundi la mashindano ya nje ya barabara yanayojulikana kama rally racing au rally raid.

Utofauti

hariri

Mbali na rallying na rally raid, kuna mashindano mengine ya nje ya barabara yanayofanana sana na enduro lakini yanatofautiana kwa kuwa hayahitaji muda maalum wa kudhibiti na mara nyingi yanatambuliwa na vyombo vingine vya usimamizi kuacha vile vya kimsingi vya enduro. Mfano mmoja nchini Marekani ni Grand National Cross Country, ambayo inafanana zaidi na hare scrambles, kama Erzberg Rodeo ya Austria kuliko Enduro, lakini iko kwenye njia fupi inayoweza kuwa maili au kilomita kadhaa kwa urefu na kurudiwa mara kadhaa. GNCC inajulikana kwa kiwango cha juu cha mashindano ya ATV (vyombo vya moto vya magurudumu manne) pamoja na mashindano ya pikipiki. Enduro ya ndani ni aina mojawapo ya enduro inayofanyika ndani ya jumba. Washiriki wanapaswa kukamilisha kwa haraka iwezekanavyo njia iliyo na vikwazo vinavyofanana na vile vilivyo katika enduro.

Wachezaji Maarufu wa Enduro

hariri
 
Juha Salminen mshindi wa mataji 12 ya dunia kwenye GP ya Italia mwaka 2008

Majeraha

hariri

Khanna et al. (2015) walifanyia uchambuzi wa fasihi kuhusu majeraha ya michezo kwa waendesha pikipiki za enduro, na kugundua: "Viungo vya mwili ndio sehemu zinazoumia zaidi katika enduro. Hata hivyo, 98% ya majeraha haya ni ya wastani au madogo." Kwa kuwa kulikuwa na tafiti nne tu kuhusu majeraha ya pikipiki za nje ya barabara, walikamilisha kwa kusema: "Kuna uhaba wa data zilizochapishwa kuhusu majeraha ya enduro. Uelewa wa kina wa kipengele cha kisaikolojia cha waendesha pikipiki wa enduro, na ufuatiliaji wa karibu wa majeraha, unahitajika ili kukuza hatua za usalama katika enduro na kupunguza hatari za majeraha ambazo kwa upande wake zitasaidia kufanya enduro kuwa mbadala na salama kwa michezo mingine hatari ya pikipiki."

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Enduro". americanmotorcyclist.com. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Brief History of Enduro, Enduro 411, AMA Western Checkpoint Enduro Championship, retrieved 20 February 2012
  3. "AMA Enduro Racing rulebook". nationalenduro.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Riding Your First Enduro". dirtrider.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Association, American Motorcyclist. "Getting Started in Enduro", American Motorcyclist Association. Retrieved on 2024-11-21. (en-US) Archived from the original on 2018-08-26. 
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Enduro kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Story 1