Gang Starr
Gang Starr lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lenye athira kubwa ya East Coast hip hop. Kundi linaunganisha watu wawili, ambao ni MC Guru na DJ/mtayarishaji DJ Premier. Kundi hilo lilijulikana sana kwa staili ya aina yao, ambayo inajumlisha baadhi ya elementi za hip hop na swing jazz ya New York.
Gang Starr | |
---|---|
DJ Premier na Guru
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Boston, Massachusetts Brooklyn, New York |
Aina ya muziki | Hip hop Jazz rap Alternative hip hop |
Miaka ya kazi | 1987 - 2005 |
Studio | Wild Pitch Chrysalis Noo Trybe Records Virgin |
Ame/Wameshirikiana na | Gang Starr Foundation |
Wanachama wa zamani | |
Guru DJ Premier |
Historia
haririKundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1986 na Guru (baadaye akaja kujulikana kama Keithy E. The Guru) na DJ 1,2 B-Down (pia anajulikana kama Mike Dee) na watayarishaji kadhaa, kama vile Donald D, J.V. Johnson au DJ Mark the 45 King naye alisaidia kuanzishwa kwa kundi hili. Mnamo 1987 na 1988, Gang Starr wakatoa single ya kwanza iliyofanyika katika studio za Wild Pitch label.
Mnamo 1989, kundi likasambaratika na wanachama pekee waliotaka kuliendeleza kundi wakapendekeza jina la Gang Starr, na huyo alikuwa Guru. Baadaye akapata kuwasiliana na DJ Premier (baadaye akajakujulikana kama Waxmaster C) ambaye alimtumia tepu ya biti iliyompendeza Guru. Baada ya kuipata biti, akaona bora amwalike DJ Premier ili aungane na Gang Starr na katika mwaka huohuo wakatoa single yao iliyokwenda kwa jina la "Words I Manifest" ikiwa sambamba na albamu iliyopewa jina la "No More Mr. Nice Guy" (1989).
Wakati wa shughuli zao Gang Starr walisaidia kuvumbua sauti ya hip hop ya New York. Matoleo yote ya Gang Starr, hasa Step in the Arena (1991), Daily Operation (1992) "Hard to Earn" (1994) na Moment of Truth (1998) zilipata heshima kubwa saana. Wimbo wa "Jazz Thing", uliokuwemo kwenye filamu ya Spike Lee ya Mo' Better Blues, ilisaidia kuinua sauti ya jazz rap.
Gang Starr Foundation
haririHali ya sasa
haririDiscografia
hariri- No More Mr. Nice Guy
- Imetolewa: 1989
- Billboard 200 chati: -
- R&B/Hip-Hop chati: 83
- Mauzo ya U.S.: 53,000[1]
- Single: "Words I Manifest"/"DJ Premier In Deep Concentration"/"Here's The Proof", "Positivity"/"No More Mr. Nice Guy (Remix)"
- Step in the Arena
- Imetolewa: 15 Januari 1991
- Billboard 200 chati: 121
- R&B/Hip-Hop chati: 19
- Mauzo ya U.S.: 287,000[1]
- Single: "Just To Get A Rep"/"Who's Gonna Take The Weight?", "Love Sick"/"What You Want This Time?"/"Credit Is Due", "Step In The Arena"/"Check The Technique (Remix)"/"Credit Is Due"
- Mass Appeal: Best of Gang Starr
- Imetolewa: 26 Desemba 2006
- Billboard 200 chati:
- R&B/Hip-Hop chati:
- Single:
- Gang Starr appeared on the Brand New Heavies 1992 album "Heavy Rhyme Experience, Vol. 1 " with a track called "It's Gettin' Hectic"
Marejeo
haririViungo vya Nje
hariri- Year Round Records Ilihifadhiwa 6 Agosti 2005 kwenye Wayback Machine. DJ Premier's label site
- Guru - Who he's worked with + discography Ilihifadhiwa 11 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.
- DJ Premier - Who he's worked with + discography Ilihifadhiwa 3 Septemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- "Jazz and Hip-Hop" Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine. by Jared Pauley, (Jazz.com Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine.)
- Whatever Happened To Gang Starr (Cartoon) Ilihifadhiwa 26 Mei 2009 kwenye Wayback Machine.