Geji (kutoka neno la Kiingereza gauge, hasa track gauge au rail gauge) ni umbali kati ya pau mbili za feleji kwenye njia ya reli. Upana hupimwa baina ya pande za ndani za pau.

Matumizi ya geji tofauti duniani

Nchi nyingi hutumia geji sanifu ya milimita 1,435 (au futi 4 na inchi 8 1/2). Nchi nyingine huwa na geji pana zaidi, nyingine tena na geji nyembamba zaidi. Geji nyembamba zinasababisha gharama ndogo kuliko geji pana.

Kwa reli za pekee zisizounganishwa na mtandao wa njia za reli wa taifa kuna pia geji tofautitofauti. Kwa jumla mizigo mizito sana huelekea kutumia geji pana, na kwa mizigo myepesi geji nyembamba zinatosha.

Katika Afrika ya Mashariki njia za reli zilijengwa awali kwa geji nyembamba ya mita 1.

Geji mbalimbali

hariri

Takriban asilimia 55 za njia za reli duniani hutumia geji sanifu. Njia za reli zenye geji tofauti zinapokutana ni lazima kuwa na vituo vya kubadilisha magurudumu ya mabehewa, vinginevyo treni haziwezi kuendelea.

Geji Jina Urefu wa njia zao (kilomita) Matumizi
1000mm Geji ya mita km 95,000 Argentina (km 11000), Brazil (km 23489), Bolivia, Chile ya kaskazini, Uswisi , Afrika ya Mashariki, sehemu za Afrika ya Magharibi
(takriban asilimia 7% ya njia zote za reli duniani
1067mm (futi 3 inchi 6) km 112,000 Afrika ya Kusini, Nigeria, Indonesia, Japan, Taiwan, Ufilipino, New Zealand, Queensland, Western Australia
(takriban asilimia 9% ya njia zote za reli duniani
1435mm Geji sanifu km 720,000 Albania, Argentina, Australia, Austria, Ubelgiji, Bosnia na Herzegovina, Bulgaria, Canada, China, Kroatia, Kuba, Ucheki, Denmark, Djibouti, Ethiopia, Ufaransa, Ujerumani, Great Britain (Ufalme wa Maungano), Ugiriki, Hungary, reli za mjini Uhindi , Indonesia, Italia, Israel, Liechtenstein, Luxemburg, Macedonia Kaskazini, Mexico, Montenegro, Uholanzi, Korea Kaskazini, Norwei, Panama, Peru, Ufilipino, Poland, Romania, Serbia, Slovakia, Slovenia, Korea Kusini, Spain, Uswidi, Uswisi, Marekani, Uruguay, Venezuela, pia reli za binafsi huko Japani na reli ya mkasi mkuu Taiwan.
(takriban asilimia 55% ya njia zote za reli duniani
1520mm Geji ya Kirusi km 220,000 Armenia, Azerbaijan, Belarus, Ufini, Estonia, Georgia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Latvia, Lithuania, Moldova, Mongolia, Russia, Tajikistan, Turkmenistan, Ukraine, Uzbekistan.
(takriban asilimia 17.2% za reli zote za dunia)
1524mm Geji ya Ufini km 5,865 Ufini (inapatana na milimita 1520)
1600mm Geji ya Ireland km 9,800 Eire, Eire ya Kaskazini (Ufalme wa Maungano) (km 1800), huko Australia hasa Victoria na sehemu za Australia Kusini (km 4017), Brazil (km 4057)
1668mm Geji ya Iberia km 15,394

1. | Ureno, Hispania. Hispania huwa na km 11,683 za geji hii, na pia km 22 za geji za mchanganyiko manmo 2010.[1] Ureno shirika la Rede Ferroviária Nacional (REFER) linaendesha km 2,650 za geji hii.[1]

1676mm Geji ya Uhindi km 134,008 India, Pakistan, Bangladesh,Sri Lanka, Argentina, Chile, BART huko Marekani San Francisco Bay Area
(takriban asilimia 11.37% ya njia zote za reli duniani
 
Reli ndogo za aina hii hutumiwa katika migodi zikiwa na geji nyembamba
 
Reli hii fupi inabeba magari hata malori kwenye mtelemko wa mlima nchini Austria; geji yake ina mita 8.2, ni geji pana kabisa duniani

Kwa jumla urefu wa njia kwa kila aina ya geji:

Geji Urefu wa njia(km) Asilimia ya njia zote za reli
Geji pana 385,067 29.3%
Geji sanifu 720,000 54.8%
Geji nyembamba 207,000 15.8%

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 Karl Arne Richter (editor), Europäische Bahnen '11, Eurailpress, Hamburg, 2010, ISBN 978-3-7771-0413-3

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • A history of track gauge Archived 4 Desemba 2008 at the Wayback Machine. by George W. Hilton
  • "Railroad Gauge Width". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-17. Iliwekwa mnamo 2017-05-23. — A list of railway gauges used or being used worldwide, including gauges that are obsolete.
  • The Days they Changed the Gauge in the U.S. South
  • Juan Manuel Grijalvo - The Myth of the "Standard" Gauge
  NODES