Gervais Yao Kouassi

Gervais Yao "Gervinho" Kouassi, (amezaliwa Ányama, 27 Mei 1987) ni mchezaji wa kandanda wa kimataifa wa Ivory Coast,ambaye anacheza kama mshambuliaji katika ligi ya Ufaransa Ligue 1 na klabu ya Lille OSC.

Gervinho
Maelezo binafsi
Jina kamili Gervais Yao Kouassi
Tarehe ya kuzaliwa 27 Mei 1987
Mahala pa kuzaliwa    Anyama, Ivory Coast
Urefu 1.79m
Nafasi anayochezea Mshambulizi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Lille OSC
Namba 27
Klabu za vijana
1998–2002
2002–2004
2004–2005
ASEC Abidjan
Toumodi
KSK Beveren
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2005–2007
2007–2009
2009–
KSK Beveren
Le Mans
Lille OSC
Timu ya taifa
2007&ndash Ivory Coast

* Magoli alioshinda

Miaka ya awali

hariri

Gervinho alizaliwa katika eneo la Ányama, mji sawa kama mshambulizi wa Sevilla na wa kimataifa wa Ivory Coast Arouna Koné.

Alianza kazi yake katika shule ya vijana maarufu ya soka ya ASEC Abidjan, ambapo alikuwa huko kwa miaka mitano. Baada ya hapo, alihamia I timu ya ligi ya Ivory Coast ya Deuxiemme Daraja la Nne,Toumodi F.C..Ibrahim Toure,kaka yao Yaya na Kolo Toure kutoka timu za Barcelona na Manchester City alikuwa huko pia kwa muda fulania akicheza.

Baada ya misimu miwili saa Toumodi, akaifuata nyayo ya wachezaji wa Ivory Coast na akaenda timu ya ligi ya Ubelgiji,KSK Beveren. Alicheza huko mpaka mwisho wa msimu wa 2006/07 alipohamia ligi ya Ufaransa ya Ligue 1 kuchezea timu ya Le Mans.Huku,alicheza pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast,Romaric.

 
Gervinho akicheza katika timu ya Lille OSC

Hapo Mei 2008,baada ya kuwa na msimu wa kucheza soka unaovutia akiwa Ligue 1,iliripotiwa kuwa mshambulizi huyu alikuwa akifuatiliwa na timu kama AS Monaco,Paris-St.Germain,Marseille na hata timu ya ligi kuu ya Uingereza,Arsenal. Ripoti ilisema kuwa Arsenal,timu yenye makao yake jijini London walikuwa wamevutiwa na Gervinho kwa muda mrefu, akiwa amepewa nafasi ya kuungana nao alipokuwa akicheza nchini Ubelgiji.

Gervinho amehusishwa sana na kuhamia Arsenal. Gervinho alielezea hamu yake ya kuhamia timu hiyo,ikithibitisha uvumi kuwa Arsenal walikuwa wanamtaka. Alisema angeendelea kufanya kazi kwa bidii huko Le Mans kisha Arsenal itamfungulia milango. Hivi majuzi,Tottenham Hotspur wamekuwa wakijaribu kufikia mpango mwema na Le Mans ya kumhamisha Gervinho hadi timu hiyo ya Meneja Redknapp. Le Mans wakatangaza kwamba kama Gervinho alikuwa anaenda kokote,wangetaka £ milioni 5.5,hata hivyo Redknapp bado anamtaka katika timu yake akiwa pamoja na Giovanni Dos Santos. Tarehe 21 Julai 2009:mshambulizi huyu wa Ivory Coast alihamia timu ya Lille OSC kutoka Le Mans UC72,kwa mkataba wa miaka mitatu.Bei ya Uhamisho ilikuwa euro milioni 8.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Gervinho alikuwa nahodha wa timu ya Olimpiki ya Ivory Coast. Katika mwezi wa Septemba 2007,yeye alifunga bao kutoka mkwaju wa penalti na kufanya washinde timu ya mali kwa mabao 3-1 ili kuhitimu kucheza katika Olimpiki ya Beijing.

Yeye alikuwa mmoja wa wachezaji katika kikosi cha taifa kilichotajwa kucheza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Angola na Qatar hapo Novemba 2007.Alichaguliwa tena kucheza katika kampeni ya kuhitimu kucheza katika Shindano la Kombe la Afrika nchini Ghana ,alikopewa jezi ya nambari 10. Yeye alicheza mechi yake ya umuhimu sana kwa timu ya taifa katika shindano hilo la huko Ghana alipoingia kama mchezaji mbadala mara mbili.

Yeye iliwakilisha nchi yake katika mashindano ya Olimpiki ya 2008. Alifunga bao moja na kumsaidia mchezaji mwingine kuweza kufunga bao katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Serbia.Hivi sasa anashiriki katika Shindano la Kombe la Afrika la 2010 nchini Angola.Alicheza katika mechi dhidi ya Burkina Faso ambapo walitoka sare tasa 0-0.

Viungo vya nje

hariri
  1. Gervinho Archived 6 Mei 2009 at the Wayback Machine.
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gervais Yao Kouassi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
iOS 1
mac 6
os 11