Ghuba ya Biskaya
Ghuba ya Biskaya (kwa Kiingereza: Bay of Biscay) ni ghuba kubwa ya Atlantiki ya kaskazini-magharibi inayopakana na Ufaransa na Hispania.
Jina linatokana na nchi ya Wabaski wanaoishi pande zote mbili za mpaka wa nchi hizo.
Ghuba ya Biskaya inajulikana kwa dhoruba kali na mawimbi makubwa yaliyosababisha ajali nyingi za meli. Siku hizi usalama umeboreshwa kwa msaada wa teknolojia ya kisasa.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ghuba ya Biskaya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |