Guantanamo Bay au Hori ya Guantanamo (kwa Kihispania Bahía de Guantánamo) ni hori ya Bahari ya Karibi inayoingia kusini mwa kisiwa cha Kuba yenye upana wa km 20 na urefu wa km 8.

Mahali pa Guantánamo Bay katika Kuba
Ramani ya Guantánamo Bay
Wafungwa walipofika mwaka 2002

Kituo cha Kijeshi cha Marekani

Historia ya kituo

Ni pia jina la kituo cha kijeshi cha Marekani chenye eneo la km² 117,6 kilichopo kwenye kisiwa cha Kuba. Eneo hili lilikodishwa na Kuba kwa Marekani mwaka 1903 kwa muda wa miaka 99. Wakati ule Kuba ilitwaliwa na wanajeshi Wamarekani baada ya Vita ya Marekani dhidi Hispania ya 1898. Marekani ilidai kibali cha Kuba kwa utawala kwake juu ya Guantanamo Bay kama sharti kabla ya kuondoa jeshi lake.

Kwa sababu hiyo serikali ya Kuba ya mapinduzi ya 1958 haikutambua tena mapatano haya kwa sababu inadai Kuba ililazimishwa kijeshi kukubali.

Matumizi ya kituo

Marekani imejenga bandari ya kijeshi pamoja na uwanja wa ndege na huwa na kikosi cha askari 9,500. Kuna ukuta na fensi ya kutenganisha kituo na maeneo chini ya serikali ya Kuba.

Kambi ya wafungwa maalumu tangu 2001

Tangu mwaka 2001 kambi la wafungwa limejengwa kituoni lenye mnamno wafungwa 1,000 hasa kutoka Afghanistan waliokamatwa baada ya mashambulio ya kigaidi ya 11 Septemba 2001 katika Marekani na vita katika Afghanistan iliyofuata. Marekani ilipeleka hapa watu waliokamatwa Afghanistan na penginepo duniani wanaoshtakiwa kuwa magaidi wa Al-Qaida au Taliban lakini ambao hawakuwa bado na kesi mbele ya mahakama.

Utaratibu huu ni nje ya sheria za Marekani na haulingani na sheria za kimataifa kuhusu kuwatendea wafungwa wa vitani.

Nchi nyingi dunani zimepinga kuwepo kwa makambi haya na kudai wafungwa watendewe ama kama wafungwa wa vita au kupelekwa mahakamani kama magaidi.

Mwaka 2007 ni bado zaidi ya wafungwa 500 kambini.

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guantanamo Bay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES