James Milner

Mchezaji mpira wa Uingereza

James Philip Milner (alizaliwa Januari 4, 1986) ni mchezaji wa soka wa Uingereza ambaye anachezea klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Liverpool F.C. na timu ya taifa ya Uingereza. Milner anaweza kucheza nafasi mbalimbali kama vile beki wa kulia, kiungo na winga.

James Milner akiwa Liverpool (2022).
James Milner akiwa Aston Villa (2009)

Kipaji cha Milner katika mpira wa miguu, kriketi, na mbio ya umbali mrefu kilitambulika akiwa na umri mdogo sana. Aliwakilisha shule yake katika michezo.

Mnamo mwaka 1996, alijiunga na chuo cha vijana wa Leeds United. Alicheza kwanza kwa timu ya kwanza mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 16 tu na alipata umaarufu kama mchezaji mdogo zaidi wa kwanza kufunga goli katika Ligi Kuu.

Wakati akiwa Leeds United, alihamia Swindon Town ili kupata uzoefu kama mchezaji wa timu ya kwanza. Baadae alihamia Newcastle United,na baadae tena alikopwa na Aston Villa kwa msimu.

Aliendelea kucheza Newcastle, kabla ya kurudi Aston Villa kwa uhamisho wa kudumu mwaka 2008. Mnamo Juni 4, 2015, Milner alikubali kujiunga na Liverpool kwa uhamisho wa £ milioni 20 kutoka Manchester City. Tarehe 7 Agosti 2015, Milner alitangazwa kuwa nahodha msaidizi. Kisha mwaka 2023 akajiunga na Brighton & Hove Albion mpaka sasa.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Milner kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

[[Jamii:{{ #if:1986|Waliozaliwa 1986|Tarehe ya kuzaliwa

  NODES