James Watt (19 Januari 1736 - 19 Agosti 1819) alikuwa mhandisi kutoka Uskoti. Amekuwa maarufu kwa kuboresha injini ya mvuke kufikia kiwango kilichowezesha matumizi ya mashine hii kwa viwanda. Kwa njia hiyo alikuwa katiy a watu waliweka msingi kwa mapinduzi ya viwanda wa karne ya 18 na karne ya 19.

James Watt
Sampuli ya injini ya mvuke ya James Watt

Mafunzo yake

hariri

Alizaliwa Uskoti katika familia ya kipresbiteri kama mtoto wa mjenzi wa meli. Shuleni alipenda hisabati na kusoma mengi lakini lugha na historia aliacha kando. Angependa kuwa daktari lakini wazazi walishindwa kumgharamia masomo ya chhuoni. Alipofikia umri wa miaka 17 aliingia katika mafunzo ya fundi makanika huko London. Aliamwacha fundi mwalimu alipoona hajifunzi kitu kipya tena bila kusubiri kutimiza miaka saba ya kawaida na kwa sababu hiyo hakutambuliwa kama fundi kamili.

Fundi wa Chuo Kikuu cha Glasgow

hariri

Watt alibahatika alipopata kazi ya fundi kwa vifaa vya upimaji kwenye chuo kikuu cha Glasgow. Alipendwa na walimu na wanafunzi waliokutana katika karakana ndogo ya Watt kwa majadiliano. Profesa wa fizikia Joseph Black na mwanauchumi Adam Smith wakawa marafiki zake.

Mwaka 1760 Watt alimwoa Margaret Miller. Kati ya watoto wao ni mwanawe James pekee aliyeishi kufikia umri mkubwa.

Kukutana na injini ya mvuke

hariri

Mwaka 1764 rafiki mwingine Profesa John Robison alimwonyesha injini ya mvuke. Watt alianza kusoma yote juu ya teknolojia hii yaliyopatikana kwake. Chuo kikuu kilikuwa na injini moja iliyoharibika na Watt alipewa kazi ya kuitengeneza. Alifaulu lakini aliona ya kwamba injini ilikuwa na tatizo la muundo wake kwa sababu kiasi kikubwa cha nishati kilipotea badala ya kufanya kazi.

Jitihada za kubuni injini mpya

hariri

Watt alitengeneza sampuli ndogo ya injini bora. Marafiki kwenye chuo kikuu walimsaidia kwa kumpa pesa alipotengeneza injini kubwa. Utengenezaji wa mashine hizi ulikuwa na matatizo makubwa. Wafanyakazi wa wakati ule hawakuzoea kutekjeleza shughuli kwa umakinifu uliohitajika kwa mashine hii. Mtajiri aliyomsaidia kwa pesa alishindwa kuendelea na mwenye kiwanda mwingine aliingia akiamini ubora wa muundo wa Watt.

Ilichukua miaka kadhaa na msaada wa watu mbalimbali hadi injini ya mvuke iliyoboreshwa ilikuwa tayari kwa uzalishaji na matumizi. Tangu 1785 kiwanda cha Watt na mwenzake kilianza kuleta faida ya kifedha na hali yake ya kiuchumi kilikuwa nzuri.

Watt aliendelea kutengezea aina mpya za gia kwa mashine yake iliyowezesha matumizi yake kwa shughuli nyingi. Alibuni pia kizio cha kupima nguvu akaiita "nguvu ya farasi" (horsepower) kinachoendelea kutumiwa duniani kama kipimo kwa nguvu ya injini hata kama kipimo kipya cha SI kinachoitwa "Watt" (wati) kimechukua nafasi yake kitaalamu.

  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Watt kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1