Jimbo la Rasi
Jimbo la Rasi lilikuwa kubwa kati ya majimbo manne ya Afrika Kusini kabla ya 1994. Lilianzishwa mwaka 1910 wakati Koloni ya Rasi ilipoingia katika Muungano ya Afrika Kusini pamoja na majimbo ya Natal, Transvaal na Dola Huru la Oranje. Mji mkuu wa jimbo ulikuwa Cape Town.
Katika miaka ya 1960 maeneo ya bantustan Bophuthatswana, Transkei na Ciskei zilitengwa na jimbo.
Katiba mpya ya 1994 illeta mpangilio mpya ya utawala na eneo la Jimbo la Rasi likagaawiwa na kuingia katika majimbo mapya ya Rasi ya Magharibi (Western Cape), Rasi ya Kaskazini, Rasi ya Mashariki (Eastern Cape) na Kaskazini-Magharibi.