Kangaruu
Jike la kangaruu kijivu mashariki (Macropus fuliginosus) akiwa na ndama wake kwenye pochi
Jike la kangaruu kijivu mashariki (Macropus fuliginosus) akiwa na ndama wake kwenye pochi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Marsupialia (Wanyama wanaobeba watoto wao ndani ya pochi ya ngozi))
Oda: Diprotodontia (Wanyama wenye meno makubwa mawili mbele kwa mdomo)
Nusuoda: Macropodiformes (Wanyama kama kangaruu)
Familia: Macropodidae (Wanyama walio na mnasaba na kangaruu)
Nusufamilia: Macropodinae (Wanyama wanaofanana na kangaruu)
Gray, 1821
Ngazi za chini

Spishi 4:

Kangaruu (kutoka Kiingereza: kangaroo) ni jina la wanyama mamalia wa spishi mbalimbali walio wenyeji wa Australia. Wote ni wala majani wanaobeba watoto wao wachanga ndani ya pochi ya ngozi iliyopo nje ya mwili juu ya tumbo wakiwa spishi zinazojulikana zaidi ya wanyama wa ngeli ndogo ya marsupialia. Familia ya spishi zao huitwa kwa jina la biolojia Macropodidae yaani wenye miguu mikubwa (kwa Kigiriki makrós (kubwa) na poús (mguu)). Familia hiyo ina spishi takriban 60.

Dume la kangaruu mwekundu (Macropus rufus) huko Taronga Western Plains Zoo, Australia

Kwa matumizi ya kawaida neno hili hutumika kuelezea spishi hii kutoka kwenye familia kubwa hasa wale wa jenasi ya Macropus, kangaruu mwekundu, kangaruu wa kijivu wa magharibi na kangaruu wa kijivu wa mashariki [1]. Kangaruu ni wazawa wa bara la Australia. Jamii nyingine kangaruu wengine wanapatikana pia Australia na New Guinea.

Kangaruu wakubwa wamezoea mabadiliko yaliyosababishwa na kilimo cha kibinadamu katika mazingira yao asilia lakini wale wa spishi za wadogo wengi wapo hatarini. Hawafugwi kwa lolote lakini kangaruu wa mwituni wanawindwa kwa ajili ya nyama, michezo na kulinda malisho ya kondoo na ng'ombe [2] japo kwa vipingamizi. Uwindaji wa kangaroo una faida kubwa kimazingira na kiafya kwa ngombe na kondoo wanaochungwa kwa ajili ya nyama.[3]

Kangaroo ni alama ya taifa ya Australia picha yake inatumika katika ngao ya taifa [4], kwenye pesa zake[5] na baadhi ya mashirika makubwa ya Australia.[6] Kangaroo ni muhimu sana kwa utamaduni na sura ya taifa ya Australia.

Maelezo

hariri
 
Kangaruu kijivu mashariki akikimbia

Kuna spishi nne ambazo huonwa kuwa kama ni kangaruu.

  • Macropus giganteus, Kangaruu Kijivu Mashariki (Eastern grey kangaroo) hawafahamiki sana nje ya Australia lakini huonekana sana hasa maeneo ya mashariki mwa bara.
  • Macropus fuliginosus, Kangaruu Kijivu Magharibi (Western grey kangaroo) huyu ni mdogo kiasi,karibu kg, 54 kwa dume mkubwa hupatikana mashariki mwa Australia, kusini mwa Australia na kwenye bonde la mto Darling.
  • Osphranter antilopinus, Kangaruu Swala (Antilopine kangaroo) kwa uhalisia, wanapatikana kaskazini zaidi ukilinganisha na wengine kama wao, ni viumbe wa nyikani na msituni na huishi kwa makundi makundi.
  • Osphranter rufus, Kangaruu Mwekundu (Red kangaroo) ndiye mkubwa kuliko wengine wote wachache kwa idadi na hupatikana kwenye sehemu kama kidogo za bara, dume mkubwa huweza kufikia hata urefu wa mita 2 na uzito wa kg 90.
  • Osphranter robustus, Kangaruu Imara (Common wallaroo) ni mdogo kuliko spishi tatu zilizotajwa hapa juu lakini imara zaidi. Anatokea Australia mzima lakini spishi hii imegawanywa katika nususpishi nne zinazotokea katika sehemu mbalimbali za nchi. Rangi zake zinaenda kutoka hudhurungi kupitia kahawianyenkundu hadi kijivu iliyoiva.
  • Osphranter bernardus, Kangaruu Mweusi (Black wallaroo) ni mdogo kabisa wa spishi zote za kangaruu na ana msambazo mdogo kabisa kwenye Arnhem Land, Northern Territory. Madume wana rangi ya kahawia iliyoiva sana au nyeusi, huku majike wakiwa kahawiakijivu.

Zaidi kuna wanyama wengine wadogo zaidi wanaohusiana kwa ukaribu na kangaruu kwenye familia Macropodidae.

 
Kangaruu mwekundu (Macropus rufus)

Kwa muda mrefu Ulaya ilimuona kangaroo kama mnyama wa ajabu watu wa mwanzo walisema kuwa kangaroo wanakuwa kama tandala (bila ya pembe); amesimama kama binadamu na anaruka kama chura. Kangaroo wana miguu ya nyuma yenye nguvu, maalumu kwa ajili ya kuruka, mkia mrefu wa nyuma wenye misuli kwa ajili ya balance, na kichwa kidogo, kangaroo jike huwa na mfuko (masupilim) ambamo mtoto humalizia kukua akiwa humo ndani.

Kangaroo ndio wanyama pekee wakubwa wanao jongea kwa kuruka. Mwendo kasi wake wa kuruka kwa kawaida ni km 20 - 25 kwa saa na anaweza kukimbia mpaka kwa kilometa 70 kwa saa kwa umbali mfupi, japo anaweza kukimbia kwa kilometa 40 kwa saa kwa hata kilometa mbili.[7] Mwendo huu umezoeleka kwake kwa sababu yeye si tu kukimbia maalum, lakini mara nyingi hukimbia kutafuta chakula na maji.

Kwa sababu ya wayo zake kubwa hawawezi kutembea vizuri na kwa kasi ndogo. Anatumia mkia wake na miguu ya mbele,kuweka kiegemeo cha miguu mitatu na kasha husogeza miguu yake miwili mikubwa. [8] Kangaruu huishi kwa miaka mine au sita (4-6). [9]

Chakula

hariri
 
Kangaruu kijivu mashariki porini

Kangaruu hula nyasi na majani ya vichaka, spishi ndogo za kangaruu hula fungi. Spishi nyingi huchanganyika usiku[10] na hutumia muda mwingi wa mchana kupumzika kivulini, na kutembea kutafuta chakula jioni tulivu, usiku na asubuhi. Kwa sababu ya ulaji wake meno ya kangaroo yamejifanyia meno mengine maalum. Meno yake chonge yanauwezo wa kung’ata nyasi chini kabisa karibu na ardhi na magego yake kwa ajili ya nyasi.mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kama ya chakula usio toa gesi ya methane. Licha ya kuwa na utaratibu wa mfumo wa mmengenyo wa chakula kama wa wanyama wengine wala nyasi, mfano ngombe ambao hutoa kiasi kikubwa cha methane; wakati wa kutoa hewa kangaruu hawatoi nje gesi ya methane. Hewa ya hidrojeni badala ya kuwa methane, hubadilishwa na huwa kemikali ya aseteki, ambayo hutumika kutengeneza nishati zaidi. Wanasayansi wa mimea wanashauku kubwa ya kubainisha bakteria wanaofanya kazi hiyo toka kwa kangaroo mpaka kwa ng'ombe sababu gesi ya methane hutoka kwa ng'ombe. Ng’ombe huchangaia uchafuzi wa hali ya hewa mara 23 zaidi kuliko hewa ya ukaa.

Kuyamudu mazingira

hariri
 
Ndama mchanga wa kangaruu akinyonya ndani ya mfuko
 
Kangaruu mtoto

Kangaruu wamejijengea maungo kadhaa yanayo wawezesha kuishi katika makazi yasiyo na rutuba na hali ya hewa yenye kubadilika badilika Bila kutegemewa wakati wa ukame msimu usio wa mvua, Ngamia dume hawazalishi manii, nao kangaroo jike hushika mimba tu kama kuna mvua ya kutosha ya kuzalisha kiasi kikubwa cha majani.

Kuna mahusiano wakati wa kuruka na kupumua kwa kangaroo wakati mguu unatoka ardhini hewa inatoka mapafuni kurusha mguu mbele tayari kwa kutua hujaza tena mapafu kwa hewa kuweka matumizi mazuri ya nishati, uchunguzi umeonesha kuwa zaidi ya nishati inayotumika kuvukia kangaroo huhitaji nishati ndogo sana kama anataka kuvuka sana tofauti na wanyama wengine wanapoongeza kasi ya miendo yao mf. farasi na binadamu

Uzazi na mzunguko wa uzazi

hariri

Yai la kangaroo jike huwa ndani ya ovari na hushuka mpaka kwenye uterasi tayari kwa ajili ya kurutubishwa.kijusi hukua kwa haraka sana na kutoka nje baada ya siku 33, kwa kawaida huwa anazaliwa mtoto mmoja tu. Mtoto huyo huwa haoni hana nywele na urefu wa sentimeta chache sana miguu yake ya nyuma huwa inakuwa haijakuwa hivyo hutumia tu miguu ya mbele kujisogeza kwenye mfuko wa mama yake, na huchukua dakika tatu mpaka tano. Akifika ndani ya pochi huanza kunyonya. Baada ya siku 150, mtoto anaweza kutokeza nje kwa mara ya kwanza. Baada ya kuchunguila chungulia nje kwa siku kadhaa na kuona kuwa ni salama. Baada ya hapo hutumia muda wake mwingi kuchungulia nje duniani na baada ya siku 235, hutoka nje ya pochi kwa mara ya mwisho. [11]

Nyama ya kangaroo hupikwa kwa namna mbalimbali. Nyama hii tena ni chakula kwa wakazi asili wa Australia.

Tanbihi

hariri
  NODES
todo 1