Karoli Borromeo (2 Oktoba 15383 Novemba 1584) alikuwa kardinali na askofu mkuu wa Milano nchini Italia.

Karoli Borromeo

Aliongoza jimbo hilo kubwa kama mchungaji halisi tena makini kwa mahitaji wa Kanisa la wakati wake: aliitisha na kuongoza sinodi mbalimbali, alianzisha seminari kwa ajili ya malezi ya waklero, alitembelea mara kadhaa kundi lake lote ili kustawisha maisha ya Kikristo akatoa sheria nyingi ili kuokoa milele watu [1].

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 4 Novemba[2].

Maisha

hariri

Karoli Borromeo alizaliwa katika mji wa Arona katika mkoa wa Lombardia nchini Italia mwaka 1538.

Baada ya kupata shahada ya tatu katika sheria za serikali na za Kanisa, alifanywa kardinali na mjomba wake, Papa Pius IV, akachaguliwa kuwa askofu mkuu wa Milano.

Hata hivyo aliishi maisha magumu ya kifukara, hata alifananishwa kwa mbwa katika nyumba ya bwana wake.

Alikuwa mchungaji bora wa kundi lake. Mara kwa mara alipitia parokia zote jimboni mwake, aliitisha mikutano, hasa sinodi 11, aliweka sheria za kufaa kwa watu, na alijitahidi kuhimiza maadili ya Kikristo.

Alitoa huduma nyingi kwa maskini, kama vile shule za bure, mabweni, nyumba za wasichana ili kuwatoa katika ukahaba, n.k.

Ndiye aliyefanikisha zaidi sehemu ya mwisho wa Mtaguso wa Trento na utekelezaji wake, kama vile uanzishaji wa seminari kwa ajili ya malezi ya mapadri wapya.

Alianzisha pia shirika la Oratorio jimboni mwake.

Alifariki dunia tarehe 3 Novemba 1584.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1562
  • A. Sala, Documenti circa la vita e la gesta di Borromeo (4 vols., Milan: 1857–1859)
  • Chanoine Silvain, Histoire de St Charles Borromeo (Milan: 1884)
  • A. Cantono, "Un grande riformatore del secolo XVI" (Florence: 1904); "Borromus" in Herzog-Hauck, Realencyklopädie (Leipzig: 1897).

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES
mac 3
os 1