Kaskazini-Magharibi (jimbo la Afrika Kusini)

Jimbo la Kaskazini-Magharibi
Bokone Bophirima
North West Province
Eneo 116 320 km²
Wakazi (2001) 3 669 349
Lugha Kitswana (65.4%)
Kiafrikaans (7.5%)
Kixhosa (5.9%)
Kisotho (5.7%)
Kitsonga (4.7%)
Kisepedi (4.2%)
Kizulu (2.5%)
KiNdebele (1.3%)
Kiingereza (1.2%)
Wakazi kimbari Waafrika Weusi(91.5%)
Wazungu(6.7%)
Chotara(1.6%)
Wenye Asili ya Asia (0.3%)
Mji Mkuu Mafikeng
Waziri Mkuu Supra Mahumapelo (ANC)
Mahali pa Kaskazini-Magharibi

Kaskazini-Magharibi ni jimbo la Afrika Kusini. Mji mkuu ni Mafikeng. Jimbo liliundwa baada ya mwisho wa siasa ya Apartheid (yaani ubaguzi wa rangi wa kisheria) kutokana na sehemu za majimbo ya awali ya Transvaal na Jimbo la Rasi pamoja na sehemu kubwa ya Bantustan ya Bophuthatswana.

Jiografia

hariri

Jimbo limepakana na nchi ya Botswana na majimbo yafuatayo ya Afrika Kusini:

Eneo lake ni km² 116,190.

Wakazi

hariri

Mwaka 2001 wakazi 3,669,349 walihesabiwa. Idadi kubwa ni Watswana na Kitswana ni lugha ya kwanza jimboni. Lugha ya pili ni Kiafrikaans.

Mji mkubwa ni Mafeking iliyounganishwa na Mmabatho (awali mji mkuu wa Bophuthatswana). Miji mingine yenye maana ni Potchefstroom, Klerksdorp, Brits, Rustenburg, Lichtenburg na Vryburg.

Uchumi

hariri

Migodi na uchimbaji madini huzalisha theluthi moja ya pato la jimbo. Zaidi ya 90% ya platini ya Afrika Kusini inapatikana karibu na Rustenburg na Brits. Pia robo ya dhahabu ya Afrika Kusini imepatikana jimboni.

Upande wa kilimo kuna hasa mahindi na mavuno yake ni theluthi ya mavuno ya taifa. Mazao mengine ni pamoja na alizeti, matunda, tumbako na pamba. Sehemu za magharibi na kaskazini zinafaa kwa ufugaji wa kondoo.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kaskazini-Magharibi (jimbo la Afrika Kusini) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 2