Kibwagizo cha filamu

Kibwagizo cha filamu (kutoka Kiingereza: film score) ni muziki unaopigwa hasa nyuma ya filamu (ambao hasa unatofautishwa na zile nyimbo zinazotumika ndani ya filamu). Istilahi ya kibwagizo cha filamu katika Kiswahili ipo moja tu kwa maana mbili, lakini katika Kiingereza ipo tofauti kidogo. Kwa mfano, istilahi ya neno "soundtrack" haichanganywi na film score (ingawa mara kwa mara huchanganywa). Istilahi ya "soundtrack" pia hujumlisha kitu chochote cha sauti ndani ya filamu kama vile vionjo vya sauti na mazungumzo ya kujibizana (dialogue). Albamu ya soundtrack au vibwagizo pia inaweza kujumlisha nyimbo zilizokuwepo kwenye filamu vilevile miziki iliyotolewa hapo awali na wasanii wengine. Istilahi ya score hutungwa hasa kwa ajili ya kuisindikiza filamu, na mtunzi halisi wa vibwagizo vya filamu.

Viungo vya Nje

hariri
  NODES
Association 1
INTERN 2
Note 2