Kihindi (Devanagari: हिन्दी au हिंदी) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya nchini Uhindi, Nepal, Afrika Kusini na Singapuri inayozungumzwa na Wahindi. Ni lugha ya kitaifa nchini Uhindi. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kihindi nchini Uhindi imehesabiwa kuwa watu milioni 258; tena kuna watu milioni 120 ambao huitumia lugha ya Kihindi kama lugha ya pili au ya mawasiliano. Wengine husema kwamba kinaeleweka kati ya theluthi mbili ya Wahindi wote yaani takriban watu milioni 650, na wasemaji wa Kihindi kama lugha ya kwanza ni zaidi ya milioni 180. Pia kuna wasemaji 361,000 nchini Afrika Kusini (2003), wasemaji 77,600 nchini Nepal (2011) na wasemahi 13,100 nchini Singapuri (2010). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kihindi iko katika kundi la Kiaryan au la lugha za Kihindi-Kiajemi. Lugha za karibu ni pamoja na Kipunjabi, Kisindhi, Kigujarati, Kimarathi na Kibengali.

Lugha imetoka katika Sanskrit ya kale iliyokuwa lugha ya chanzo cha utamaduni wa Uhindi.

Kihindi, Kiurdu na Kihindustani

hariri

Kihindi ni umbo la lugha ya Kihindustani nchini India. Kihindustani ilikuwa jina la pamoja katika Uhindi wa kaskazini kabla ya ugawaji wa mwaka 1947 mwisho wa ukoloni na kuanzishwa kwa nchi huru za Pakistan na India. Baada ya uhuru lugha ya pamoja ya awali iliitwa "Kihindi" upande wa India na "Kiurdu" upande wa Pakistan. Hali halisi lugha hizi mbili ni kama lugha 1 hata kama Urdu huandikwa kwa herufi za Kiarabu na Kihindi kwa herufi za Devanagari.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kihindi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES