Kitabu cha Yoeli ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh.

Nabii Yoeli alivyochorwa na Michelangelo kwenye dari ya Kikanisa cha Sisto IV (15081512).

Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Muda wa uandishi

hariri

Inawezekana kwamba kitabu hiki kilikuwa cha mwisho kuandikwa kati ya vitabu vya kinabii vya Biblia ya Kiebrania (ambamo Kitabu cha Danieli, kilichoandikwa baadaye, hakimo katika kundi la Manabii).

Mwandishi wake ni nabii Yoeli, labda katikati ya karne ya 4 KK.

Muhtasari

hariri

Katika sura mbili za kwanza, uvamizi wa nzige unaharibu mkoa wote wa Yudea na kuwafanya wenyeji waendeshe liturujia ya toba ambayo iliitikiwa na Mungu kwa ahadi ya kusamehe na kurudisha hali njema.

Katika sura mbili zinazofuata unatabiriwa kwa mtindo wa kiapokaliptiko hukumu ya mataifa ya kigeni na ushindi wa moja wa moja wa Mungu na taifa lake, Israeli.

Mwangwi katika Agano Jipya

hariri

Mtume Petro alitaja utabiri wa Yoeli akieleza karama zilizojitokeza siku ya Pentekoste ya mwaka 30 BK kutokana na ujio wa Roho Mtakatifu (taz. Yoe 3:1-5 na Mdo 2:16-21).

Mtume Paulo alitumia utabiri huohuo kuhusu Wayahudi na watu wa mataifa mengine pia (taz. Yoe 3:5 na Rom 10:13).

Marejeo

hariri
  • Achtemeier, Elizabeth. Minor Prophets I. New International Biblical Commentary. (Hendrickson, 1999)
  • Ahlström, Gösta W. Joel and the Temple Cult of Jerusalem. Supplements to Vetus Testamentum 21. (Brill, 1971)
  • Allen, Leslie C. The Books of Joel, Obadiah, Jonah & Micah. New International Commentary on the Old Testament. (Eerdmans, 1976)
  • Anders, Max E. & Butler, Trent C. Hosea–Micah. Holman Old Testament Commentary. (B&H Publishing, 2005)
  • Baker, David W. Joel, Obadiah, Malachi. NIV Application Commentary. (Zondervan, 2006)
  • Barton, John. Joel & Obadiah: a Commentary. Old Testament Library. (Westminster John Knox, 2001)
  • Birch, Bruce C. Hosea, Joel & Amos. Westminster Bible Companion. (Westminster John Knox, 1997)
  • Busenitz, Irvin A. Commentary on Joel and Obadiah. Mentor Commentary. (Mentor, 2003)
  • Calvin, John. Joel, Amos, Obadiah. Calvin’s Bible Commentaries. (Forgotten Books, 2007)
  • Coggins, Richard. Joel and Amos. New Century Bible Commentary. (Sheffield Academic Press, 2000)
  • Crenshaw, James L. Joel: a New Translation with Introduction and Commentary. The Anchor Bible. (Yale University Press, 1995)
  • Finley, Thomas J. Joel, Amos, Obadiah: an Exegetical Commentary. (Biblical Studies Press, 2003)
  • Garrett, Duane A. Hosea, Joel. The New American Commentary. (B&H Publishing, 1997)
  • Hubbard, David Allen. Joel and Amos: an Introduction and Commentary. Tyndale Old Testament Commentary. (Inter-Varsity Press, 1990)
  • Limburg, James. Hosea–Micah. Interpretation – a Bible Commentary for Teaching & Preaching. (Westminster John Knox, 1988)
  • Mason, Rex. Zephaniah, Habakkuk, Joel. Old Testament Guides. (JSOT Press, 1994)
  • McQueen, Larry R.M. Joel and the Spirit: the Cry of a Prophetic Hermeneutic. (CTP, 2009)
  • Ogden, Graham S. & Deutsch, Richard R. A Promise of Hope–a Call to Obedience: a Commentary on the Books of Joel & Malachi. International Theological Commentary (Eerdmans/ Hansel, 1987)
  • Ogilvie, John Lloyd. Hosea, Joel, Amos, Obadiah, Jonah. Communicator's Commentary 20. (Word, 1990)
  • Price, Walter K. The Prophet Joel and the Day of the Lord. (Moody, 1976)
  • Prior, David. The Message of Joel, Micah, and Habakkuk : Listening to the Voice of God. The Bible Speaks Today. (Inter-Varsity Press, 1999)
  • Pohlig, James N. An Exegetical Summary of Joel. (SIL International, 2003)
  • Roberts, Matis (ed). Trei asar : The Twelve Prophets : a New Translation with a Commentary Anthologized from Talmudic, Midrashic, and Rabbinic Sources. Vol. 1: Hosea. Joel. Amos. Obadiah. (Mesorah, 1995)
  • Robertson, O. Palmer. Prophet of the Coming Day of the Lord : the Message of Joel. Welwyn Commentary. (Evangelical Press, 1995)
  • Simkins, Ronald. Yahweh's Activity in History and Nature in the Book of Joel. Ancient Near Eastern Texts & Studies 10 (E. Mellen Press, 1991)
  • Simundson, Daniel J. Hosea–Micah. Abingdon Old Testament Commentaries. (Abingdon, 2005)
  • Stuart, Douglas. Hosea–Jonah. Word Biblical Commentary 31. (Word, 1987)
  • Sweeney, Marvin A. The Twelve Prophets, Vol.1: Hosea–Jonah. Berit Olam – Studies in Hebrew Narrative & Poetry. (Liturgical Press, 2000)
  • Wolff, Hans Walter. A Commentary on the Books of the Prophets Joel & Amos. Hermeneia – a Critical and Historical Commentary on the Bible. (Augsburg Fortress, 1977)

Viungo vya Nje

hariri
Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Yoeli kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1
eth 2
Story 1