Kwando (au: Cuando; kabla ya mdomo pia Linyanti halafu Chobe) ni mto wa Afrika ya Kusini na tawimto la Zambezi. Chanzo chake kiko nyanda za juu za Bié (Angola) inapoelekea kusini-mashariki. Inakuwa mpaka kati ya Angola na Zambia kwa km 140, halafu inapita Kishoroba cha Caprivi na kuwa mpaka kati ya Namibia na Botswana.

Mto Kwando (Cuando)
Mto Kwando (kushoto) unaingia Mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula (kulia katikati)
Chanzo Nyanda za juu za Bié (Angola)
Mdomo Mto Zambezi kwa mji wa Kazungula (Zambia)
Nchi Angola, Zambia, Namibia, Botswana
Urefu km 1,500
Kimo cha chanzo m 1,700 hivi
Mkondo ??
Eneo la beseni km² 96,778

Inaingia katika mabwawa wa Linyanti yenye km² 1,425. Katika sehemu hizo mto huitwa Chobe au Liyanti.

Kwa jina la Chobe unaingia katika mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula pale ambapo nchi nne za Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe zinapokutana.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kwando kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES