Laurenti (kwa Kilatini "Laurentius"; Valencia au Huesca, Hispania, 225 hivi - Roma, Italia, 10 Agosti 258) alikuwa shemasi mkuu wa Kanisa la Roma hadi alipouawa kwa kubanikwa kutokana na imani yake katika Yesu.

Laurenti mbele ya Valerianus.
Kifodini cha Mt. Laurenti kilivyochorwa na Tintoretto, Christ Church, Oxford, Uingereza.
Kifaa kinachosadikiwa kilitumika kumbanika Laurenti mjini Roma.
Jiwe ambapo maiti yake ililazwa huko Roma (San Lorenzo fuori le mura)
"Kifodini cha Mt. Laurenti" kilivyochongwa na Juan de León (1758). Kazi hii iko Real Academia de Bellas Artes de San Fernando, Madrid, Hispania.

Laurenti alikuwa msimamizi wa mali ya Kanisa la Roma iliyotumiwa kwa ajili ya kuwasaidia maskini. Serikali ya Kaisari Valerian iliwahi kumwua askofu wa Roma Sixtus II ikadai sasa Laurenti atoe hazina yote ya Kanisa kwa serikali ya Kaisari katika muda wa siku tatu. Laurenti alitumia muda huo kugawa pesa zote kwa maskini.

Akitamani kushiriki kifodini cha askofu wake, anavyosimulia Papa Leo I, siku alipotakiwa kufika mbele ya afisa wa serikali kukabidhi pesa alikuja pamoja na kundi kubwa la maskini, wagonjwa, walemavu, vipofu, wenye ukoma, wajane na mayatima. Halafu kwa dhihaka alimwambia akida, "Hao ndio hazina ya Kanisa". Akida alimtesa na kumfunga kwenye nondo za chuma juu ya moto hadi alikufa. Inasemekana ya kwamba Laurenti alivumulia mateso kimyakimya akisema mwishoni, "Ewe mtu maskini, kwangu moto huu umepoa lakini kwako utaleta maumivu ya milele". Alizikwa katika shamba la Mungu la Verano ambalo mpaka leo linaitwa jina lake[1].

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu mfiadini, hasa siku ya kifodini chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES
mac 3
os 3