Lysippo
Lysippo (kwa Kigiriki: Λύσιππος) alikuwa mchoraji wa Kigiriki wa karne ya 4 KK. Pamoja na wachongaji wengine Scopas na Praxiteles, anahesabiwa kuwa mmoja wa wachongaji wakubwa wa Ugiriki ya Kale. Ni vigumu kutafiti kazi za Lysippos na kutambua mtindo wake kutoka kwenye nakala za kkazi zake ambazo zipo hadi sasa.
Lysippo alizaliwa huko [Sicyon] karibu na mwaka 390 KK. Akiwa kijana, alikuwa mfanyakazi zinazohusiana na [[shaba]. Alijifunza mwenyewe sanaa ya kuchonga, baadaye akawa mkuu wa shule ya Argos na Sicyon. Kulingana na mwanahistoria Pliny, Lysippo alitengeneza kazi zaidi ya 1,500 za shaba. Mwanafunzi wake, Chares wa Lindos, ndiye aliyejenga Sanamu Kubwa ya Rhodes, ambayo ni mojawapo ya Maajabu Saba ya Dunia ya Kale. Sanamu hii haipo tena hivi sasa.
Viungo vya Nje
hariri- Wasifu wa Lysippo Archived 19 Agosti 2017 at the Wayback Machine.
- Kuhusu Lysippo toka Britannica
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lysippo kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |