Marburg ni mji wa Hesse nchini Ujerumani, makao makuu ya wilaya ya Marburg-Biedenkopf (Landkreis). Mji huo unaenea kando ya mto Lahn.

Marburg

Nembo
Nchi Ujerumani
Jimbo Hesse
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 79.454
Tovuti:  www.marburg.de
Marburg.

Idadi ya wakazi wake ni takriban 79.454. [1]

Historia

hariri

Ilipokea hati ya haki ya mji mnamo mwaka 1222. Baadaye ilikuwa mji mkuu wa utemi wa kujitegemea wa Hessen-Marburg wakati wa karne za 16 - 17.

Mnamo mwaka 1527 Chuo Kikuu cha Marburg kiianzishwa kama chuo cha Kiprotestanti.

Marburg ni pia kitovu kimojawapo cha tasnia ya dawa nchini Ujerumani. Ugonjwa wa Marburg ulitambuliwa mara ya kwanza hapa katika maabara. Kuna pia kiwanda cha dawa ya kampuni ya BioNTech inayotoa dawa za Covid-19.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Population of major towns in Hesse, Germany". Statista.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Marburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
mac 2