Melchior Ndadaye (28 Machi 1953 - 21 Oktoba 1993) alikuwa msomi wa sayansi na mwanasiasa. Yeye alikuwa wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia na wa kwanza wa kabila la Wahutu kuwa rais wa Burundi baada ya kushinda uchaguzi kuu wa kihistoria mwaka 1993.

Melchior Ndadaye

Melchior Ndadaye, 1993

Muda wa Utawala
10 Julai 1993 – 21 Oktoba 1993
Waziri Mkuu Sylvie Kinigi
mtangulizi Pierre Buyoya
aliyemfuata François Ngeze

tarehe ya kuzaliwa (1953-03-28)28 Machi 1953
Nyabihanga, Ruanda-Urundi
(saga Burundi)
tarehe ya kufa 21 Oktoba 1993 (umri 40)
Bujumbura, Burundi
mahali pa kuzikiwa Bujumbura
chama Front for Democracy in Burundi (FRODEBU)
Burundi Workers' Party (UBU)
ndoa Laurence Ndadaye
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda
Hifadhi ya Kitaifa ya Sanaa na Ufundi

Ingawa alijaribu kukomesha ukabila katika nchi hiyo, marekebisho yake yalishawishi askari katika jeshi lililotawaliwa na Watutsi, na aliuawa katikati ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa mnamo Oktoba 1993, baada ya miezi mitatu tu ofisini.

Kuuliwa kwake kulizua idadi ya mauaji ya kikatili baina ya makabila ya Watutsi na Wahutu, na mwishowe yalizua Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi vilivyodumu muongo mzima.

Mwaka 2020 mtangulizi wake Pierre Buyoya na wenzake wengi walihukumiwa kwenda jela maisha kwa kumuua.[1]

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Melchior Ndadaye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES