Mikoa ya Tanzania
Tanzania imegawiwa katika mikoa 31, ikiwemo 26 upande wa bara na 5 upande wa Zanzibar.
Tanzania |
Makala hii imepangwa kwa mfululizo: |
|
|
Nchi zingine · Atlasi |
Mikoa ya Tanzania, miji mikuu, eneo na idadi ya wakazi
Mkoa | Makao makuu |
Wilaya | Eneo (km2) |
Idadi ya Wakazi[1] |
Msimbo wa posta |
Kanda |
---|---|---|---|---|---|---|
Arusha | Arusha | 7 | 34,516 | 2,356,255 | 23xxx | Kaskazini |
Dar es Salaam | Dar es Salaam | 5 | 1,393 | 5,383,728 | 11xxx | Pwani |
Dodoma | Dodoma | 7 | 41,311 | 3,085,625 | 41xxx | Kati |
Geita | Geita | 5 | 20,054 | 2,977,608 | 30xxx | Ziwani |
Iringa | Iringa | 5 | 35,503 | 1,192,728 | 51xxx | Nyanda za Juu za Kusini |
Kagera | Bukoba | 8 | 39,627 | 2,989,299 | 35xxx | Ziwani |
Katavi | Mpanda | 3 | 45,843 | 1,152,958 | 50xxx | Nyanda za Juu za Kusini |
Kigoma | Kigoma | 8 | 45,066 | 2,470,967 | 47xxx | Kati |
Kilimanjaro | Moshi | 8 | 13,209 | 1,861,934 | 25xxx | Kaskazini |
Lindi | Lindi | 6 | 67,000 | 1,194,028 | 65xxx | Pwani |
Manyara | Babati | 6 | 47,913 | 1,892,502 | 27xxx | Kaskazini |
Mara | Musoma | 7 | 31,150 | 2,372,015 | 31xxx | Ziwani |
Mbeya | Mbeya | 7 | 60,350 | 2,343,754 | 53xxx | Nyanda za Juu za Kusini |
Morogoro | Morogoro | 7 | 70,799 | 3,197,104 | 67xxx | Pwani |
Mtwara | Mtwara | 7 | 16,707 | 1,634,947 | 63xxx | Pwani |
Mwanza | Mwanza | 7 | 9,467 | 3,699,872 | 33xxx | Ziwani |
Njombe | Njombe | 6 | 21,347 | 889,946 | 59xxx | Nyanda za Juu za Kusini |
Pemba Kaskazini | Wete | 2 | 574 | 272,091 | 75xxx | Zanzibar |
Pemba Kusini | Chake Chake | 2 | 332 | 271,350 | 74xxx | Zanzibar |
Pwani | Kibaha | 7 | 32,407 | 2,024,947 | 61xxx | Pwani |
Rukwa | Sumbawanga | 4 | 22,792 | 1,540,519 | 55xxx | Nyanda za Juu za Kusini |
Ruvuma | Songea | 5 | 66,477 | 1,848,794 | 57xxx | Nyanda za Juu za Kusini |
Shinyanga | Shinyanga | 5 | 18,901 | 2,241,299 | 37xxx | Ziwani |
Simiyu | Bariadi | 5 | 25,212 | 2,140,497 | 39xxx | Ziwani |
Singida | Singida | 6 | 49,437 | 2,008,058 | 43xxx | Kati |
Songwe | Vwawa | 5 | – | 1,344,687 | – | Nyanda za Juu za Kusini |
Tabora | Tabora | 7 | 76,151 | 3,391,679 | 45xxx | Kati |
Tanga | Tanga | 10 | 27,348 | 2,615,597 | 21xxx | Kaskazini |
Unguja Kaskazini | Mkokotoni | 2 | 470 | 257,290 | 73xxx | Zanzibar |
Unguja Mjini Magharibi | Jiji la Zanzibar | 2 | 230 | 893,169 | 71xxx | Zanzibar |
Unguja Kusini | Koani | 2 | 854 | 195,873 | 72xxx | Zanzibar |
Mikoa hiyo yote imegawanyika tena kwenye wilaya 169. Wilaya zimeganyika katika kata kibao.
Historia ya mikoa
Ugawaji wa nchi wakati wa ukoloni
Utawala wa Kijerumani
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani eneo la Tanzania Bara (=Tanganyika) lilikuwa pamoja na Rwanda na Burundi kama Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mwaka 1913 eneo lote liligawiwa kwa mikoa 21 na maeneo matatu ya wawakilishi wakazi. Mikoa 19 ilikuwa chini ya wakuu wa mkoa wa kawaida yaani maafisa raia Wajerumani (jer. Bezirksleiter au Bezirkamtsmann) waliyemwakilisha gavana na mikoa miwili ilikuwa chini ya mamlaka ya kijeshi yaani afisa wa jeshi la kikoloni la schutztruppe.
Mikoa ya kawaida ilikuwa:
Na. | Mkoa | Na. | Mkoa |
---|---|---|---|
1. | Wilhelmstal (Lushoto) | 11. | Langenburg (Tukuyu) |
2. | Tanga | 12. | Bismarckburg (Kasanga) |
3. | Pangani | 13. | Ujiji |
4. | Bagamoyo | 14. | Tabora |
5. | Morogoro | 15. | Dodoma |
6. | Dar es Salaam | 16. | Kondoa-Irangi |
7. | Rufiji | 17. | Moshi |
8. | Kilwa | 18. | Arusha |
9. | Lindi | 19. | Mwanza |
10. | Songea |
Mikoa miwili ya Iringa na Mahenge ilikuwa "mikoa ya kijeshi" yaani chini ya usimamizi ya maafisa wakuu wa jeshi la Schutztruppe.
Maeneo ya Bukoba (takriban sawa na Mkoa wa Kagera wa leo), Ruanda na Urundi yaliendelea kutawaliwa na watawala wao wa kienyeji wakiangaliwa na mwakilishi mkazi wa Ujerumani aliyekuwa kama balozi, mshauri mkuu na msimamizi wa watawala hao.
Utawala wa Kiingereza
Tangu mwaka 1918/1919 eneo la Tanganyika lilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa Uingereza bila maeneo ya Rwanda (Ruanda) na Burundi (Urundi). Tanganyika ikigawiwa mwaka 1922 kuwa na mikoa ileile ilhali majina ya Kijerumani yalibadilishwa kuwa majina ya kienyeji kama vile [2]:
Arusha, Bagamoyo, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa (si tena mkoa wa kijeshi), Kilwa, Kondoa-Irangi, Lindi, Mahenge (si tena mkoa wa kijeshi), Morogoro, Moshi, Mwanza, Pangani, Rufiji, Rungwe, Songea, Tabora, Tanga, Ufipa (badala ya Bismarckburg), Ujiji na Usambara (badala ya Wilhelmstal).
Katika miaka iliyofuata mfumo huo wa kiutawala ukabadilishwa. Mnamo mwaka 1948 Waingereza walikuwa na majimbo ("provinces") yafuatayo[3]:
Na. | Jimbo | Idadi ya wakazi | |
---|---|---|---|
1. | Central (Kati) | 821,147 | |
2. | Eastern (Mashariki) | 933,120 | |
3. | Lake (Ziwani) | 1,853,719 | |
4. | Northern (Kaskazini) | 592,300 | |
5. | Southern (Kusini) | 917,648 | |
6. | Southern Highlands
(Nyanda za Juu za Kusini) |
849,995 | |
7. | Tanga | 557,245 | |
8. | Western (Magharibi) | 952,503 | |
Tanganyika yote | 7,477,677 |
Mwaka 1961 Jimbo la Mashariki likagawiwa na Dar es Salaam kuwa jimbo la pekee. Ziwa Magharibi ikatengwa na Mkoa wa Ziwani.
Nyakati za uhuru
Majimbo hayo 10 yalirithiwa na nchi huru ya Tanganyika.
Tarehe 26 Aprili 1964 Tanganyika na Zanzibar zikaungana. Tanzania sasa ilikuwa na majimbo 12. Majimbo hayo yalibadilishwa mnamo 1966 kuwa mikoa 20.
Na. | Jimbo | Idadi ya Wakazi | Eneo (km²) | Makao makuu | Mikoa ya baadaye | |
---|---|---|---|---|---|---|
1. | Kati | 886,962 | 94,301 | Dodoma | Dodoma, Singida | |
2. | Mashariki | 955,828 | 107,630 | Dar es Salaam | Pwani (kisehemu), Morogoro | |
3. | Dar es Salaam | 128,742 | 1,393 | Dar es Salaam | Pwani (kisehemu) | |
4. | Ziwani | 1,731,794 | 107,711 | Mwanza | Mara, Mwanza, Shinyanga (kisehemu) | |
5. | Ziwa Magharibi | 514,431 | 28,388 | Bukoba | Ziwa Magharibi | |
6. | Kaskazini | 772,434 | 85,374 | Arusha | Arusha, Kilimanjaro (kisehemu) | |
7. | Kusini | 1,014,265 | 143,027 | Mtwara | Mtwara, Ruvuma | |
8. | Nyanda za Juu za Kusini | 1,030,269 | 119,253 | Mbeya | Iringa, Mbeya (kisehemu) | |
9. | Tanga | 688,290 | 35,750 | Tanga | Kilimanjaro (kisehemu), Tanga | |
10. | Magharibi | 1,062,598 | 203,068 | Tabora | Kigoma, Mbeya (kisehemu), Shinyanga (kisehemu), Tabora | |
11. | Zanzibar | 165,253 | 1,658 | Zanzibar | Zanzibar Shambani, Zanzibar Magharibi | |
12. | Pemba | 133,858 | 984 | Chake Chake | Pemba | |
Majimbo yote | 9,084,724 | 928,537 |
- Mwaka 1967 Zanzibar Shambani (Rural) ikagawiwa kuwa Zanzibar Shambani Kaskazini na Zanzibar Shambani Kusini. Mikoa hiyo iliitwa baadaye Kaskazini Zanzibar na Kusini Zanzibar.
- 1971 Mkoa wa Rukwa ulianzishwa kutokana na maeneo ya Mbeya na Tabora.
- 1972 Mkoa wa Lindi ukatengwa na Mtwara.
- 1974 Mkoa wa Dar es Salaam ukatengwa na Mkoa wa Pwani
- 1982 Mkoa wa Pemba ukagawiwa kuwa Kaskazini Pemba na Kusini Pemba
- 1984 Jina la Mkoa wa Ziwa Magharibi likabadilishwa kuwa Mkoa wa Kagera
- 2002 Mkoa wa Manyara ukatengwa na Arusha,
- Mwaka 2012 mikoa minne mipya ilianzishwa ambayo ni
- Mkoa wa Geita, kutoka maeneo ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera
- Mkoa wa Katavi, awali ilikuwa Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Rukwa
- Mkoa wa Njombe, kutoka maeneo ya Mkoa wa Iringa (wilaya za Ludewa, Makete na Njombe)
- Mkoa wa Simiyu, kutoka maeneo ya mikoa ya Shinyanga (Bariadi, Meatu na Maswa) na Mwanza (Busega).
- Mwaka 2016 ulianzishwa mkoa wa Songwe kwa kumega mkoa wa Mbeya upande wa magharibi.
Tazama pia
- Orodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneo ukubwa wa mikoa kwa ujumla wa eneo, eneo la ardhi, na eneo la maji.
- Wilaya za Tanzania
Marejeo
Viungo vya nje
- https://allglobalupdates.com/list-ya-mikoa-yote-tanzania/ Ilihifadhiwa 25 Novemba 2022 kwenye Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mikoa ya Tanzania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |