Mikromita ni sehemu ya 1,000,000 ya mita moja. Alama yake ni µm. Ni sawa na sehemu ya 1,000 ya milimita moja. Inakubaliwa ndani ya muundo wa vipimo sanifu vya kimataifa.

Neno limetokana na maneno mawili ya Kigiriki μικρός (mikrós) = ndogo na μέτρον (métron) = kipimo.

Mikromita hutumiwa kama kipimo cha masafa ya mawimbi (ing. wavelength) ya mnururisho au pia katika mikrobilojia. Bakteria ya kawaida huwa na kipenyo cha mikromita 1.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mikromita kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES