Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Kitabu cha karne ya 19 kikiarifu watoto kwamba Waholanzi ni wachapakazi na Wachina ni watiifu kwa wazee.

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa.

Mila na desturi hujengwa, hukomaa, hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na pia hufifia na hatimaye huweza kupotea.

Desturi huanza kama tabia ya mtu au kundi la watu. Tabia hiyo ikienea kwa jamii nzima hugeuka kuwa desturi. Desturi zikiota mzizi zikawa ndizo mila, namna halali ya kufanya mambo. Kumbe jamii hukemea tabia mbaya ili zisisambae na kugeuka kuwa desturi.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mila kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES