Mopti (kwa Kibambara: ߡߏߕߌ ߘߌߣߋߖߊ, Moti Dineja) ni mkoa wa Mali wenye eneo la km2 79,017. Mji mkuu wake ni Mopti.

Ramani ya Mkoa wa Mopti

Wakati wa mzozo wa mwaka 2012 kaskazini mwa Mali, mpaka kati ya maeneo ya Mali yaliyodhibitiwa na serikali kuu na maeneo ya waasi katika kaskazini ulipitia Mkoa wa Mopti. [1]

Jiografia

hariri

Mkoa wa Mopti umepakana na Mkoa wa Timbuktu upande wa kaskazini, Mkoa wa Segou upande wa kusini-magharibi, na Burkina Faso upande wa kusini mashariki.

Wakati wa sensa ya mwaka 2009 idadi ya wakazi katika mkoa ilikuwa 2,037,330. Eneo hili lina makabila mbalimbali yakiwa pamoja na Wabozo, Wasonghai, Wadogon, Wafulani, Wamalinke na Wabambara.

Mto Niger unavuka eneo hilo. Kwenye mji wa Mopti unapokea maji ya tawimto lake Bani.

Maeneo makuu ndani ya mkoa ni pamoja na delta ya barani ya mto Niger karibu na Mopti, miamba ya Bandiagara na uwanda wa Bankass kwenye mpaka wa Burkina Faso. Mlima Hombori wenye kimo cha mita 1153 ni mlima mkubwa nchini Mali ukiwa karibu na Mopti mjini.

Kwa upande wa tabianchi mkoa wa Mopti unachukuliwa kuwa sehemu ya ukanda wa Sahel.

Miji mikubwa zaidi ya eneo hilo ni Mopti, Sevare (ambayo iko ndani ya manisipaa ya Mopti), Djenne, Bandiagara, Bankass, Douentza, na Youwarou .

Usafiri na uchumi

hariri

Uwanja wa ndege wa Mopti unahudumia mkoa wote, wakati Mto Niger una usafiri wa maji hadi Koulikoro na Segou kuelekea magharibi na Timbuktu na Gao upande wa mashariki.

Mkoa huu una umwagiliaji wa kutosha na kilimo chake kimeendelezwa vizuri. Uvuvi ni tawi muhimu la uchumi. Kuna utalii kwenye nchi ya Dogon na hasa katika miji ya Mopti na Djenne penye Msikiti Mkuu wa Djenne ambayo ni jengo kubwa ya udongo duniani.

Mji wa Djenne na Miamba ya Bandiagara zimepokelewa kazika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO .

Wilaya

hariri
 
Cercles za Mkoa wa Mopti

Mopti imegawanywa kwa wilaya (cercles) 8 zinazojumuisha halmashauri 108: [2]

Jina la Cercle Eneo (km2) Idadi ya watu

Sensa ya 1998

Idadi ya watu
Sensa ya 2009
Bandiagara 10,520 237,139 317,965
Benki 9,054 195,582 263,446
Djenné 4,563 155,551 207,260
Douentza 23,481 155,831 247,794
Koro 10,937 267,579 361,944
Mopti 7,262 263,719 368,512
Ténenkou 11,297 127,237 163,641
Youwarou 7,139 81,963 106,768

Kuna zaidi ya vijiji 1,000 katika Mkoa wa Mopti. [3]

Marejeo

hariri
  1. Mali: Mopti, the last frontier before Sharia law, France 24, 4 Oktoba 2012, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Januari 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Communes de la Région de Mopti (PDF) (kwa Kifaransa), Ministère de l’administration territoriale et des collectivités locales, République du Mali, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-03-09.
  3. "Villages". dogonlanguages.org. 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-02. Iliwekwa mnamo 2021-02-22.

Viungo vya nje

hariri
  NODES
languages 1
mac 1
os 1