Mlinzi (ndege)

Familia ya ndege wa bahari
Mlinzi
Mlinzi mkia-kabari
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Procellariiformes (Ndege kama walinzi)
Familia: Procellariidae (Ndege walio na mnasaba na walinzi)
Leach, 1820
Ngazi za chini

Jenasi 16:

Walinzi ni ndege wa bahari wa familia Procellariidae. Spishi za jenasi Macronectes huitwa Kwazi-bahari pia. Walinzi wanafanana na albatrosi. Kwa hivyo rangi zao zinatofautiana kutoka nyeupe kabisa kupitia nyeupe na kijivu au kahawia mpaka mwili wote mweusi. Wana domo kubwa lenye ncha kwa umbo la kulabu, lakini mirija miwili ya pua inaungana juu ya domo; ile ya albatrosi haiungani.

Kama albatrosi, walinzi huenda mbali sana wakiruka angani na spishi nyingi zinaweza kuzunguka dunia. Hawapigi mabawa sana baada ya kuruka, lakini wananyiririka kwa mabawa yaliyonyooshwa. Huwakamata ngisi, samaki na gegereka na hula takataka ya uvuvi na mizoga pia. Spishi za Puffinus na Calonectris huzamia ili kuyakamata mawindo na wanaweza kufika zaidi ya mita 50 chini ya maji. Spishi nyingine huyakamata mawindo kijuujuu. Spishi kadhaa za Pachyptila huchuja maji kwa domo pana lao ili kupata zooplanktoni.

Kwa kawaida malinzi huyatengeneza matago yao kwa visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Spishi nyingi huyatembelea makoloni yao usiku kuzuia shakwe-waporaji. Jike hulitaga yai moja tu kwa kawaida ndani ya kishimo.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri
  NODES
chat 1